Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Health»DC RUNYANGO VIJANA MJITAMBUE KATIKA AFYA NDIO MAISHA ,MJIKINGE NA MAAMBUKIZI

    DC RUNYANGO VIJANA MJITAMBUE KATIKA AFYA NDIO MAISHA ,MJIKINGE NA MAAMBUKIZI

    0
    By arushatv on December 12, 2022 Health
    Na Geofrey Stephen Arusha Tengeru 
    MKUU wa wilaya ya Arumeru,mkoani Arusha, mhandisi Richard Ruyango, amewataka vijana wilayani humo sanjari na wale  wanaosoma  kwenye vyuo , kuhakikisha wanajitambua na  kujilinda na maambukizi ya ukimwi kwa kutumia kinga wanapokuwa kwenye mahusiano.
    Mhandisi Ruyango ameyasema hayo katika chuo cha maendeleo ya Jamii Tengeru wilayani humo,wakati alipohudhulia maadhimisho ya siku ya udhibiti wa ukimwi duniani  ,ambapo kitaifa yamefanyika mkoani Lindi.
    Alisema maadhimisho hayo ambayo kiwilaya yalifanyika katika chuo hicho ,walilenga kutoa elimu zaidi kwa kuwakumbusha vijana kuwa Ukimwi bado upo na unaua hivyo nijukumu lao kama rasilimali ya taifa kujilinda na kuacha ngono uzembe.
    “Vijana kama rasilimali ya taifa tunasisitiza kuhakikisha wanajilinda kwani ukimwi bado upo na unauwa hivyo katika chuo hiki chenye vijana takribani 4000  tunaweza tukawa tunapoteza vijana watano hadi sita kila mwaka bila sababu za msingi”alisema .
    Alisema katika kipindi cha miaka 37 tangu janga la ukimwi limeingia nchini hakuna chanjo wala dawa iliyokwisha patikana ,ila dawa zilizopo nizakufubaza pekee,hivyo elimu tunayoendelea kuitoa ikawasaidie kuwakumbusha na lengo la serikali ni kuhakikisha watu wake wanabaki salama.
    Alisema kuwa wilaya ya Arumeru ina kiwango cha asilimia 1.5 cha maambukizo ya ukimwi ,hivyo alisisitiza kuendelea kutolewa kwa elimu ya ukimwi kwa vijana hususani waliopo vyuoni .
    Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya Meru Mwl.Zainabu Makwenya alisema lengo la kufanyia maadhimisho hayo katika chuo hicho ni kuwafikishia elimu hiyo  vijana walio wengi ambao ndio waathirika wakubwa wa janga la ukimwi.
    Awali mkuu wa taasisi ya maendeleo ya jamii ,dkt Bakari George alisema kuwa chuo hicho kimekuwa na utaratibu  wa kuwakutanisha wanachuo na wadau  ili kuwapatia mafunzo ya elimu ya afya ikiwemo maambukizo ya ukimwi ili kuwaimarisha  kisaikolojia.
    Alisema hadi sasa wanachuo hao wamepata mafunzo mara sita na katika maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani wanafunzi hao waliadhimisha kwa kuchangia damu na kupima afya zao
    Mwisho.
    Post Views: 69
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleHABARI KUBWA MAGAZETI YA LEO ARUSHA24TV,PANGA LA SAMIA KUPANGUA SERIKALI UPYA
    Next Article HABARI KUBWA, SAKATA LA GAMBO ? LEMA AMVAA ,MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA24TV

    Related Posts

    MIAKA 5, YA MREMBO MASIPETII MSICHANA MDOGO ALIYEJITOLEA KUSAIDIA JAMII NA KUACHA KAZI, ANAMILIKI NYUMBA YA MILLION 280

    March 11, 2023

    DKT MOLLEL ATOA MAJIBU MALALAMIKO UBOVU WA CHF.

    February 23, 2023

    APOTEZA MAISHA KWA KUCHAPWA FIMBO 70 ZA KIMASAI ! KOSA LA KUMTUKANA MAMA YAKE MZAZI MATUSI YA NGUONI

    January 10, 2023

    WAJAWAZITO WATAKIWA KUFANYA MAZOEZI.

    November 23, 2022

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.