Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»WIZARA YA ARDHI YAJIPANGA KUKUSANYA KIASI CHA SH, BILIONI 250 KWA MWAKA WA FEDHA

    WIZARA YA ARDHI YAJIPANGA KUKUSANYA KIASI CHA SH, BILIONI 250 KWA MWAKA WA FEDHA

    0
    By arushatv on November 4, 2022 Habari

     

    Na Geofrey Stephen ,ARUSHA

    KATIBU Mkuu wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi Dkt Allan Kijazi amevitaka vituo vya makusanyo ya Kodi na masulufu ya serikali,kutozifumbia macho taasisi za Serikali ambazo zinadaiwa kwa kuwa suala la ulipaji wa Kodi ni suala la kisheria na sio hiari.

    Dkt Kijazi aliyasema hayo mapema Leo jijini Arusha wakati akifungua kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa mkakati wa makusanyo ya Kodi ya pango la Ardhi Kwa kushirikiana na benki ya CRDB.

    Alisema kuwa ni muhimu kwa wamiliki wa ardhi kuhakikisha wanalipa Kodi hizo Kwa wakati ili kuruhusu utekelezaji na mikakati mbalimbali ya kiserikali iweze kufikiwa

    Aliongeza kuwa kwa Sasa vituo vya makusanyo ya Kodi vinatakiwa kuhakikisha kuwa hakuna mtu yeyote yule ambaye anaachwa hasa kwenye ukusanywaji wa Kodi na ikitokea hawajalipa ni muhimu hatua Kali na za kisheria ziweze kuchukuliwa.

    “Kodi ni suala la kisheria na sio hiari taasisi yeyote ambayo haijalipa kodi chukueni hatua kwa kuwa kutolipa Kodi ya pango ni sawa na ukiukwaji wa Sheria”aliongeza

    Kwa upande wake kamishna wa ardhi nchini, Mathew Nhongwe alisema kuwa kama wizara mwaka huu wa fedha wamejipanga katika mwaka wa fedha 2022/23 kukusanya kiasi cha sh, billion 250 tofauti na mwaka jana walikusanya sh,bilioni 130.

    Kamishna alisema wana mikakati mbalimbali ya kuendelea kukusanya Kodi ya pango la Ardhi Kwa kila mwananchi,taasisi za umma pamoja na binafsi

    Aliongeza kuwa wamejipanga kurahisisha zoezi la ulipaji tayari wa Kodi ya pango la Ardhi Kwa kushirikiana na taasisi na fedha.

    “Leo tupo na CRDB tunataka kama mtu anataka kulipia Kodi yake iwe ni rahisi kwake asitembee umbali mrefu apate huduma karibu’

    Hata hivyo taasisi za kifedha ikiwemo crdb Benk imeahidi kushirikiana bega Kwa bega na serikali kukusanya mapato yatokanayo sekta ya ardhi.

    Ends…

    Post Views: 65
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleBODI YA MIKOPO KIKAANGONI LEO ! MAGAZETI YA LEO ARUSHA24TV
    Next Article BILIONI 2.3 KUKAMILISHA UJENZI WA BWENI LA KIKE MAENDELEO YA JAMII

    Related Posts

    Tanzania na India kuendeleza Uhusiano wa Kibiashara na Uwekezaji

    March 27, 2023

    TANZANIA YAKABILIWA NA UHABA WA MABAHARIA VIJANA.

    March 27, 2023

    Marcas Ajitosa kuwania U NEC Arusha

    March 25, 2023

    VIKUNDI 47 KUPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI MOITA MONDULI

    March 24, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.