Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»Wafanyabiashara wadogo Tanzania na Kenya waeleza manufaa ya mradi wa barabara Tanga-Horohoro , wataka kuondolewa vikwazo mipakani.

    Wafanyabiashara wadogo Tanzania na Kenya waeleza manufaa ya mradi wa barabara Tanga-Horohoro , wataka kuondolewa vikwazo mipakani.

    0
    By arushatv on November 12, 2022 Habari

    mwandishi wetu,Tanga

    Wafanyabiashara wadogo katika mpaka wa Tanzania na Kenya, eneo la Horohoro na Lungalunga ,wametaka serikali za Tanzania na Kenya, kuondoa vikwazo vya kibiashara ,hasa baada ya kukamilika miundombinu ikiwepo barabara ya Tanga- Horororo.

    Barabara la lami ya Tanga- Horohoro, imejengwa na Serikali ya Marekani kupitia miradi ya malengo ya milenia(MCC).

    Wakizungumza na mwandishi habari hizi, katika mpaka huo, baadhi ya wafanyabiashara wadogo wa Kenya na Tanzania, walitaka serikali za Kenya na Tanzania, kuendelea kupunguza vikwazo ili biashara iwe rahisi zaidi baina ya nchi moja hadi nyingine, hasa ya mazao, mifugo na bidhaa za ndani.

    Joseph Mwanganya mfanyabishara mdogo wa Kenya kaunti ya Lungalunga ,alisema licha ya serikali za Afrika Mashariki kuwa na miundombinu bora mipakani lakini, bado changamoto kuwa ni vikwazo vya kibiashara.

    “sisi kama wafanyabiashara tunataka uhuru wa kufanya biashara hasa hizi ndogondogo turuhusiwe kuingia katika nchi hizi mipakani na kupitisha biashara ndogondogo hasa hizi za mazao”alisema

    Mwenyekiti wa Kitongoji cha Duga Maforoni, Horohoro, Tanzania, Zahoro Juma, alisema kwa sasa upande wa Tanzania biashara zimeimarika sana kutokana na uwepo wa barabara nzuri ambayo inarahisisha usafirishwaji wa bidhaa mbali mbali.

    “kuna vikwazo vidogovidogo vya kiforodha lakini.,kubwa biashara zinakwenda vizuri hivi sasa kutoka Tanga hadi Horororo unatumia saa moja tofauti na miaka ya nyuma tulikuwa tunatumia saa sita kwa kilomita 65 tu”alisema

    Mkuu wa mkoa wa Tanga, Omary Mgumba akizungumza na wananchi alisema serikali inajitahidi kupunguza vikwazo kwa wafanyabiashara wadogo katika mpaka huo na biashara zimeimarika sana tofauti na miaka ya nyuma.

    “wafanyabiashara wadogo tunawaruhusu kufanyabiashara kilometa 10 ndani ya Tanzania na Kenya bila vikwazo“alisema.

    Alisema hivi Sasa miundombinu imeimarika hasa barabara hivyo ni fursa kwa wafanyabiashara wadogo kuitumia na Serikali imetenga maeneo ya uwekezaji,ikiwepo maeneo ya viwanda na masoko ya bidhaa mbalimbali ikiwepo mifugo.

    MWISHO.

    Post Views: 48
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleMgogoro waibuka Burunge WMA , Kampuni ya kitalii ikitaka kuwinda Pembezoni mwa Tarangire Bodi ya wadhamini yampinga spika .
    Next Article WANANCHI WALIO VAMIWA NA TOPE LA MGODI KULIPWA FIDIA YA MAMILIONI !MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA24TV

    Related Posts

    Kamati yapitisha makadirio ya matumizi na maendeleo 2023/2024 kwa Wizara Uwekezaji Viwanda na Biashara.

    March 23, 2023

    MWANDISHI WA HABARI MAARUFU ALLAN ISACK AITAKA NAFASI YA MNEC

    March 23, 2023

    Vyombo vya Dola na wanasheria kushirikiana kutokomeza ujangili Babati

    March 22, 2023

    JIJI LA ARUSHA LATOA MIKOPO YA SHILINGI BILION 2.6 KWA VIJANA WENYE MAITAJI MAALUM NA WANAWEKE

    March 22, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.