Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Business»JIjI lA ARUSHA LATOA MIKOPO YA MillION 404.5 VIPAO MBELE WALEMAVU VIJANA NA WANAWAKE

    JIjI lA ARUSHA LATOA MIKOPO YA MillION 404.5 VIPAO MBELE WALEMAVU VIJANA NA WANAWAKE

    0
    By arushatv on November 10, 2022 Business
    Na Geofrey Stephen Arusha . 
    Jiji la Arusha limekabidhi hundi ya mkopo yenye thamani ya sh, milioni 404.5 kwa vikundi 52 vya ujasiriamali kutoka kata 25 za jiji la Arusha.
    Akiongea wakati wa kukabidhi hundi  hiyo jana, kaimu mkurugenzi wa jijj la Arusha Hargeney Chitukulo,alisema mkopo huo ni awamu ya pili kwa vikundi vya ujasiriamali.
    Alisema kati ya vikundi hivyo ,28 ni vya akina mama waliopata sh, milion 198.6 na vikundi 14 vya vijana waliopata sh, milioni 143.
    Alisema wengine walionufaika na mkopo huo usio na riba ni vikundi 10 vya walemavu ,waliopata sh, milioni 62.9.
    Chitukulo alisema kuwa mkopo  awamu ya kwanza  halimashauri  hiyo ilitoa sh,873.6 kwa vikundi 118 ,vikiwemo  108 vya wanawake waliopatiwa sh, milioni 754.6.vikundi 10 vya vijana walipatiwa sh, milioni 118.9.
    Alisema halmashauri ya jiji la Arusha imekuwa ikichangia maendeleo ya vikundi vya ujasiriamali  kama sheria inavyowataka kupitia vikundi vya ufugaji ,biashara ndogondogo na vyombo vya usafiri .
    “Tumekuwa tukiwapatia mafunzo kabla ya kupatiwa mkopo na leo watapatiwa mafunzo ya ujasiriamali wa miradi yenye tija ,uongozi na usimamizi wa miradi ,utunzaji wa kumbukumbu za fedha , urejeshaji wa mkopo ,uandaaji wa taarifa ,afya ,Lishe na Bima “
    Alisisitiza kuwa hali ya urejeshaji wa mikopo bado ni changamoto kubwa katika jiji la Arusha na hali  inayosababisha fedha nyingi kubaki kwa wakopaji na kuwanyima haki hiyo vikundi vingine vyenye uhitaji.
    Awali mkuu wa wilaya ya Arusha Said Mtanda aliwataka wakopaji kupitia vikundi vyao kuwa waadilifu na kutejesha mikopo hiyi kwa wakati.
    Mtanda alimpongeza kaimu mkurugenzi wa jiji hilo Chitukuro kwa kufanikisha kutekeleza na kutoa fedha hizo akisema hayo ni matunda ya serikali chini ya Rais Samia Suluhu yenye lengo la kuwakwamu kiuchuni wananchi wake.
    “Hakikisheni mikopo mliopewa mnarejesha kwa wakati ili vikundi vingine viweze kukopa msiende kutunia vibaya mkopo mliopewa.
    Naye mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo, alisema kuwa kuna tabia kwa halmashauri ya jiji la Arusha kuchelewesha kuweka fedha kwenye akaundi ya vikundi mara baada ya kukabidhi hundi ya mfano.
    Gambo alitaka fedha hizo zitolewe kwa wakati iili kuwapa fursa wakopaji waliojiwekea malengo kufanya biashara zao na kuanza kurejesha.
    Hata hivyo alisema kumekuwapo na baadhi ya wataalamu wa mikopo ambao wamekuwa wakidai rushwa kwa baadhi ya vikundi ili kupitisha maombi yao ya mkopo jambo ambalo lilikemewa na mkuu wa wilaya na kumtaka kaimu mkurugenzi kuhakikisha mikopo inatoka ndani ya wiki moja kama alivyoahidi.
    Ends..
    Post Views: 163
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleTAWA YASHIRIKI VIVUTIO VYA UTALII NYANDA ZA JUU KUSINI.
    Next Article CHADEMA WAISHTUKIA TUME YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA ! MAGAZETI YA LEO ARUSHA 24TV

    Related Posts

    WAZIRI MKENDA AZINDUA MKOPO WA ELIMU KUTOKA BENK YA NMB.

    March 15, 2023

    Tanzania na China Kuendeleza Uhusiano wa Kibiashara

    February 27, 2023

    RC MAKALA AISHUKURU BENKI YA NMB KUZAMINIA ZIARA YA VIONGOZI MACHINGA NA BODABODA RWANDA.

    February 4, 2023

    BANK YA UBA YAFIKA ARUSHA WAFANYA BIASHARA WAFURAIYA RIBA NAFUU

    January 20, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.