Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»Waziri kijaji Aiyakikishia Kamati ya Bunge Kufanyia kazi Mapendekezo ya Uwekezaji

    Waziri kijaji Aiyakikishia Kamati ya Bunge Kufanyia kazi Mapendekezo ya Uwekezaji

    0
    By arushatv on October 19, 2022 Habari

    Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) ameihakikishia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuwa Wizara itayafanyia kazi maelekezo, miongozo na maoni yaliyotolewa katika uanzishaji, ujenzi na uendelezaji wa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo na Eneo Maalum la Uwekezaji (EPZ) kwa ufanisi na kwa wakati.

    Waziri Kijaji ameyasema hayo alipokuwa akijumuisha maoni na mapendekezo ya Wajumbe wa Kamati hiyo wakati wa uwasilishaji wa Taarifa ya Machakato wa Uanzishwaji, Ujenzi na Uendelezaji wa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo na Eneo Maalum la Uwekezaji (EPZ), Oktoba 19 2022 katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

    Aidha, Dkt. Kijaji amewaeleza Wajumbe wa Kamati hiyo kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Sekta Binafsi katika kutekeleza jitihada mbalimbali zinazolenga kuendeleza Sekta ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ukiwemo Mradi huo wa kielelezo wa Bagamoyo ili kujenga uchumi shirikishi na kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025.

    Aidha, Wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wake Bw. Daniel Sillo walitoa maoni na mapendekezo mbalimbali  yanayolenga kuboresha utekelezaji wa mchakato wa uanzishaji, ujenzi na uendelezaji wa Mradi wa Bagamoyo ambao ni muhimu katika kukuza biashara na ujenzi wa uchumi wa taifa kwa haraka na kwa kuzingatia wawekezaji sahihi wenye uwezo wa kuwekeza nchini.

    Awali , Mkurugenzi Mkuu wa
    Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya nje EPZA Bw. Charles Itembe
    amesema lengo la uendelezaji wa mradi huo ni ujenzi wa Bandari ya kiwango cha kimataifa kama kitovu cha usafirishaji na lango la biashara ya kimataifa inayofungamana na eneo la viwanda kwa ajili ya uzalishaji na uongezaji thamani mazao mbalimbaliyanayozalishwa hapa nchini.

    Amesema Mradi huo unaotekelezwa Bagamoyo mkoani Pwani unafaida kubwa kwa Taifa ikiwemo kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi, kukiza teknolojia, ujuzi na ajira, kukuza biashara ya usafiri baharini na faida kwa kampuni wazawa, fedha za kigeni na kuongeza pato la taifa.

    Post Views: 68
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleMIKUTANO YA ADHARA KUANZA RASMI NOVEMBER MAGAZETI YA LEO ARUSHA24TV.
    Next Article Walimu 10 wapandishwa mahakamani kwa kuvujisha mitihani ya darasa 7 magazeti ya leo Arusha24Tv

    Related Posts

    SERIKALI YAFUNGIA MGODI WA GEM AND ROCK VENTURE ULIOKO MIRERANI

    March 20, 2023

    TRA CHUNYA KUSAMBAZA ELIMU YA MLIPA KODI KWA WACHIMBAJI WA DHAHABU.

    March 16, 2023

    Wizara ya Madini imefanikiwa kutaifisha madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 4 yenye thamani ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture

    March 16, 2023

    DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

    March 16, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.