Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Makala»WATANZANIA JITOKEZENI UWEKEZAJI KWENYE SEKTA YA MADINI – LEKASHINGO

    WATANZANIA JITOKEZENI UWEKEZAJI KWENYE SEKTA YA MADINI – LEKASHINGO

    0
    By arushatv on October 8, 2022 Makala

    Na Mwandishi wa A24Tv Geita .

    Kamishna wa Tume ya Madini Janet Lekashingo amewataka watanzania kujitokeza kwenye uwekezaji katika Sekta ya Madini kutokana na kuwepo kwa fursa mbalimbali kwenye mnyoyoro wa madini kuanzia uchimbaji, uchenjuaji, biashara ya madini na utoaji wa huduma kwenye migodi ya madini.

    Lekashingo ameyasema hayo kupitia kipindi cha Jambo Tanzania kilichorushwa mubashara na kituo cha televisheni cha TBC1 leo tarehe 08 Oktoba, 2022 kwenye Maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini katika Viwanja vya Bombambili mjini Geita.

    Amesema ili kuhakikisha kila mtanzania ananufaika na Sekta ya Madini, Serikali kupitia Wizara ya Madini imeweka mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuweka kanuni za Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini ili wananchi waweze kupata fursa za ajira na kutoa huduma mbalimbali kama vile vyakula, ulinzi na ajira kwenye migodi ya madini.

    Katika hatua nyingine, amewataka watanzania kuanzisha viwanda vya kutengeneza vipuri na huduma za usafiri kwenye migodi ya madini, biashara ambayo itakuwa ni endelevu hata mara baada ya kumalizika kwa uchimbaji wa madini.


    “ Zipo kampuni zinazomilikiwa na watanzania kama Blue Coast kwa ajili ya kutoa huduma za vifaa na usafiri kwenye migodi ya madini, mfano ambao ni mzuri; tunaomba wadau wengi zaidi kujitokeza ili kunufaika kwa kuwa na biashara endelevu,” amesisitiza Lekashingo.

    Awali akielezea maonesho hayo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Profesa Godius Kahyarara amesema kuwa maonesho yamekuwa na mafanikio makubwa kwani yametumika kama fursa  kwa kampuni kubwa za uchimbaji wa madini kutoa elimu ya teknolojia mpya ya uchimbaji wa madini na wananchi wengi kupata elimu kuhusu taratibu za kupata leseni za uchimbaji na biashara ya madini kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini.

    Aidha, amesema kuwa kupitia maonesho husika wachimbaji wadogo wamepata nafasi ya kujifunza teknolojia za kisasa za uchimbaji na uchenjuaji wa madini pasipo kuathiri mazingira.

    Post Views: 65
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleSerikali yaimarisha Mafunzo ya Umahiri wa bidhaa za ngozi nchini
    Next Article KILIO CHA KUPANDA GARAMA ZA MAISHA SERIKALI YASEMA NENO MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV

    Related Posts

    ASKOFU MASANGWA AKOSHWA NA MCHUNGAJI ALIYETUMIKIA KANISA KWA MIAKA34 AMEACHA ALAMA KUBWA

    February 26, 2023

    MZEE MOLLEL AZIKWA KIJIJINI KWAKE WANANCHI WAMWAGA MACHOZI WAZMIA WAKIAGA MWILI WAKE

    February 7, 2023

    WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezindua zoezi la ugawaji wa vishikwambi 293400 Kwa walimu wote nchini

    November 5, 2022

    PROFESA KIKULA AAINISHA MIKAKATI YA TUME YA MADINI KWENYE UBORESHAJI WA SEKTA YA MADINI

    October 13, 2022

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.