Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Elimu»SERIKALI KUFUFUA VITUO VYA WALIMU NCHI NZIMA

    SERIKALI KUFUFUA VITUO VYA WALIMU NCHI NZIMA

    0
    By arushatv on October 10, 2022 Elimu

    Na Mwandishi wa A24Tv

    Serikali imesema imeweka mkakati wa kufufua vituo vya walimu (Teachers Resource Centers) vya nchi nzima ili kuwawezesha walimu kupata sehemu ya kukutana na kubadilishana uzoefu pamoja na kujiendeleza kwa kujisomea

    Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda wilayani Bukombe wakati akiongea na walimu wa wilaya hiyo katika kuhitimisha Maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani ambapo amesema mbali ya kufufua vituo hivyo pia inaendelea kutoa mafunzo kazini kwa walimu.

    Prof. Mkenda amesema walimu wameandaliwa vizuri vyuoni lakini hiyo haitoshi kwa kuwa kila siku mambo yanabadilika na walimu wanapaswa kuendelea kujifunza kila mara ili kuwa na mbinu sahihi za ufundishaji kulingana na wakati.

    “Walimu wetu ni wazuri sana na wanaandaliwa vyema vyuoni lakini haitoshi tunapaswa kuhakikisha wanapata mafunzo kazini ya mara kwa mara na wizara ya elimu imetenga fedha kwa ajili ya kutoa mafunzo kazini kwa walimu,: amesema Pro. Mkenda.

    Amewataka walimu pia kutumia vituo vya Chuo Kikuu Huria kujiendeleza pamoja na kuchangamkia fursa za masomo zaidi ya elimu ya juu kufuatia ujenzi wa kampasi mpya 14 za vyuo vikuu mbalimbali zitakazojengwa na Wizara kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) katika Mikoa 14

    Aidha, amewaeleza walimu hao kuwa Serikali ipo katika kufanya mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 pamoja na
    mabadiliko ya mitaala yanayolenga katika kuhakikisha elimu bora na yenye kuzingatia Ujuzi inatolewa.

    Amewataka walimu hao kujiandaa kutekeleza mitaala itakayokuwa imefanyiwa mabadiliko kwani wao ndio nguzo kuu na kuwa Setikali imejipanga kuwandaa walimu wote nchini kutekeleza mtaala huo pindi utakapo kamilika.

    Naye Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amemwambia Waziri wa Elimu kuwa wilaya hiyo ina walimu ambao wanajituma na kufanya kazi kwa bidii bila kujali changamoto wanazokutana nazo.

    Pia Waziri Biteko amemwomba Prof. Mkenda kuipatia wilaya hiyo chuo cha VETA kwa kuwa ina shule za Sekondari ambazo kila mwaka zinazalisha wahitimu wa kidato cha nne na sita ambao wen

    gine wanaweza kujiunga na mafunzo ya ufundi.

    Mkuu wa mkoa wa Geita Martin Shigela ameishukuru Wizara ya elimu kwa kuzipatia kuupatia Mkoa wa Geita fedha Chui cha VETA cha Wilaya ya Chato na VETA ya Mkoa inaendelea inayoendelea kujengwa Wilayani Geita.

    Post Views: 139
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleKIGOGO WA CCM APASULIWA KICHWA NA MCHEPUKO ! MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA24TV
    Next Article DC MTANDA AMALIZA MGOMO WA DALADALA ! OPERESHENI SOMBA SOMBA

    Related Posts

    SHULE YA BILIONEA SANINIU LAIZER YAPATA UFADHILI MZITO WA MADAWATI NA MEZA ZA KISASA

    March 13, 2023

    Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Carolyne Nombo amewataka watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa umahiri.mkubwa

    February 28, 2023

    WIZARA YA ELIMU YATOA UFAFANUZI WALIO FUTIWA MATOKEO YA MITHIANI WA KIDATO CHA NNE

    February 9, 2023

    WANAFUNZI 170 WAPATIWA MSAADA WA VIFAA VYA SHULE KUTOKA OFISI YA MBUNGE WA JIMBO LA MONDULI.

    January 22, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.