Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Elimu»Rais Samia Awapatia jiji la Arusha Bilioni 2 Ujenzi wa Madarasa Mapya Dc Mtanda Awaonya wakuu wa Shule

    Rais Samia Awapatia jiji la Arusha Bilioni 2 Ujenzi wa Madarasa Mapya Dc Mtanda Awaonya wakuu wa Shule

    0
    By arushatv on October 6, 2022 Elimu

    Na Geofrey Stephen . Arusha

    HALMASHAURI ya jiji la Arusha imepokea kiasi cha sh,bilioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 100 vya madarasa katika shule za sekondari za jiji hilo ili ifikapo januari 2023 wanafunzi wote watakaochaguliwa kuingia kidato cha kwanza wawe wamejiunga na shule za sekondari.

    Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Arusha,Said Mtanda wakati akiongea na wakuu wa shule za serikali jijini hapa na kutoa siku 75 kuanzia leo , ujenzi wa madarasa hayo uwe umekamilika kwa kiwango na ubora unaotakiwa.

    Hata hivyo Mtanda alitahadhalisha matumizi mabaya ya fedha hizo na kuwaonya wakuu wa shule watakaoenda kinyume na maelekezo ya serikali,kwamba watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

    Mtanda alisema kwamba fedha hizo zimetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni mpango wa serikali wa kuhakikisha kila mwanafunzi anayefaulu elimu ya msingi anakwenda sekondari.

    “Rais aliahidi kuleta fedha za ujenzi wa madarasa na ametekeleza na tayari fedha hizo zipo kwenye akaunti yetu ya halmashauri ya jiji la Arusha sh,bilioni 2”

    Alizitaja shule 20 za sekondari zitazonufaika na fedha hizo ambazo tayari zimeshaingizwa kwenye akaunti zake ni pamoja na shule ya Arusha Day sh,milioni 100 madarasa(5).

    Shule zingine ni Arusha sekondari ,sh,milioni 160(8)Arusha Terat sh,milioni 140(7),Eleray sec sh,160(8),Felix Mrema sh,milioni 40(2),Kaloleni sh,mil.100(5),Kimaseki sh,mil 60(3),Lemara sh,mil.40(2) na Mkonoo sh,mil.20(1).

    Zingine ni Movaro Sec.sh,mil 40(2)Mrisho Gambo sh,mil.80(4)Muriet sh,mil 220(11),Naura sh,mil 100(5),Ngarenaro mil. 100(5),Olasiti sh,mil 100(5),Olmoth sh,mil 60 na Olorien sh,mil.20(1).

    Alitaja shule zingine kuwa ni Sinon sh,mil.280(14),Sombetini sh,mil 80(4) na Ungalimited sh,mil.100(5).

    Mkuu huyo wa wilaya alionya vikali kwa wakuu washule watakaochelewesha mradi huo ama kwenda kinyume na matumizi ya fedha hizo ,
    kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufukuzwa kazi na kifungo jela .

    “Natoa wiki moja kwa kila shule iwe imeunda kamati zake za ujenzi na lazima wakuu wa shule wawashirikishe wazazi na kamati ya shule wawaeleze uwepo wa fedha hizo”

    Alisema matumizi ya fedha hizo lazima yafuate mfumo wa serikali wa ‘force account’kwa kila darasa lijengwe kwa sh,milioni 20 .

    Awali mkurugenzi wa jiji la Arusha Hargeney Chitukulo alisema kuwa halmashauri hiyo imepokea kiasi cha sh,bilioni 2 siku tatu zilizopita na tayari zimeingizwa kwenye akaunti za shule.

    Chitukulo alisema atahakikisha madarasa yatakayojengwa yanakuwa na ubora unaohitajika na tayari ameteua msimamizi wa mradi katika kila shule zote zinazonufaika na mradi kwa ajili ya kusimamia mradi huo.

    Ends…

    Post Views: 93
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleCHADEMA WAMKALIA KOONI SPIKA TULIA WAMTAKA AJIUZULU ? MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV
    Next Article Matukio katika picha ushiriki wa tume ya madini katika maonyesho Geita

    Related Posts

    SHULE YA BILIONEA SANINIU LAIZER YAPATA UFADHILI MZITO WA MADAWATI NA MEZA ZA KISASA

    March 13, 2023

    Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Carolyne Nombo amewataka watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa umahiri.mkubwa

    February 28, 2023

    WIZARA YA ELIMU YATOA UFAFANUZI WALIO FUTIWA MATOKEO YA MITHIANI WA KIDATO CHA NNE

    February 9, 2023

    WANAFUNZI 170 WAPATIWA MSAADA WA VIFAA VYA SHULE KUTOKA OFISI YA MBUNGE WA JIMBO LA MONDULI.

    January 22, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.