Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Elimu»NYONGO APONGEZA MFUMO WA KIELETRONIKI USAISHAJI MITIHANI

    NYONGO APONGEZA MFUMO WA KIELETRONIKI USAISHAJI MITIHANI

    0
    By arushatv on October 30, 2022 Elimu

    Na WyEST,
    DAR ES SALAAM.

    Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imepongeza Wizara ya Elimu na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kwa kuwa na mfumo wa kielektroniki wa usahihishaji mitihani ambao umerahisisha zoezi la usahihishaji mitihani ya Taifa.

    Pongezi hizo zimetolewa Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Stanslaus Nyongo wakati Kamati ilipofanya ziara katika Taasisi hiyo ambapo mfumo huo kwa sasa unatumika kusahihisha mitihani ya darasa la Saba na Ualimu.

    Kamati hiyo pia imeishauri Wizara kuwatambua kitaifa Watanzania waliovumbua mfumo huo kutokana na kuwa umejibu changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kufupisha muda wa usahihishaji.

    “Huu uvumbuzi unatakiwa ulindwe na muone namna bora ya kuwatambua Kitaifa wavumbuzi wa mfumo huu pamoja na kuubiasharisha kwani Watanzania wengi wana imani kubwa na utendaji kazi wake uliofanikiwa kupunguza malalamiko kwa kiasi kikubwa,” amesema Mhe. Nyongo.

    Kamati hiyo imetoa maoni na mapendekezo ya kuimarisha utendaji ikiwemo kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya kutosha vitakavyowezesha mfumo huo kutumika Kikanda ili kurahisisha zaidi zoezi la usahihishaji mitihani.

    Akiongea kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga (Mb) ameishukuru Kamati hiyo kwa kutembelea NECTA na kuahidi kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na Kamati hiyo.

    Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya NECTA, Prof. William Anangisye amesema kuwa kwa sasa wataalamu wanaendelea kuandaa mifumo kwa ajili ya usahihishaji wa mitihani ya Darasa la Nne na ile ya Sekondari.

    Post Views: 63
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleKUFA AU KUISHI UAMUZI NI WAKO !MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV
    Next Article Makamu wa Rais Zanzibar Anena kuelekea Uzinduzi wa Matokeo ya Sensa

    Related Posts

    SHULE YA BILIONEA SANINIU LAIZER YAPATA UFADHILI MZITO WA MADAWATI NA MEZA ZA KISASA

    March 13, 2023

    Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Carolyne Nombo amewataka watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa umahiri.mkubwa

    February 28, 2023

    WIZARA YA ELIMU YATOA UFAFANUZI WALIO FUTIWA MATOKEO YA MITHIANI WA KIDATO CHA NNE

    February 9, 2023

    WANAFUNZI 170 WAPATIWA MSAADA WA VIFAA VYA SHULE KUTOKA OFISI YA MBUNGE WA JIMBO LA MONDULI.

    January 22, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.