Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA KUJENGA VYUO VYA VETA 62 WILAYANI .

    WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA KUJENGA VYUO VYA VETA 62 WILAYANI .

    0
    By arushatv on September 7, 2022 Habari

     

    Na Mwandishi wa A24Tv .

    Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatarajia kuanza ujenzi wa vyuo vya VETA katika Wilaya 62 ambazo hazina vyuo hivyo.

    Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga (Mb) katika kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii cha uwasilishaji wa utekelezaji wa mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko 19 kilichofanyika Septemba 6, 2022 Jijini Dodoma

    Mhe. Kipanga ameieleza Kamati hiyo kuwa katika Mwaka wa Fedha 2022/23 Wizara imetenga jumla ya Shilingi bilioni 100 ambazo zitawezesha kujenga majengo muhimu katika vyuo hivyo ili kuviwezesha kuanza kutoa mafunzo katika maeneo hayo.

    “Kwenye bajeti ya Wizara ya mwaka huu wa fedha tumetenga Shilingi bilioni 100 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa majengo muhimu katika Wilaya zote ambazo bado hazina vyuo vya VETA ili vianze kutoa mafunzo,” amefafanua Mhe. Kipanga.

    Ameongeza kuwa vyuo hivyo vikikamilika vitawezesha Wilaya zote nchini kuwa na vyuo vinavyotoa mafunzo ya ufundi na ufundi stadi ambapo mpaka sasa tayari kuna vyuo 73 vikiwemo vya Wilaya na mikoa.

    Naye Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Stanslaus Nyongo (Mb) amesema Kamati imeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo na kuipongeza Wizara.

    Amesema katika taarifa iliyotolewa kwa Kamati inaonyesha miradi yote iliyokuwa katika Mradi wa UVIKO 19 imekamilika kwa zaidi ya asilimia 90 jambo ambalo linaonyesha kuwa imekamilika kwa kiwango kikubwa.

    Post Views: 46
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleKILIO KINGINE TOZO YA MAEGESHO YA MAGARI ! MAGAZETI YA LEO ARUSHA24TV
    Next Article LISU KUREJEA TANZANIA MIAKA MITANO IMEPITA TOKA AONDOKE ! MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA24TV

    Related Posts

    SERIKALI YAFUNGIA MGODI WA GEM AND ROCK VENTURE ULIOKO MIRERANI

    March 20, 2023

    TRA CHUNYA KUSAMBAZA ELIMU YA MLIPA KODI KWA WACHIMBAJI WA DHAHABU.

    March 16, 2023

    Wizara ya Madini imefanikiwa kutaifisha madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 4 yenye thamani ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture

    March 16, 2023

    DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

    March 16, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.