Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»WATOTO 93,218 KUPATIWA CHANJO JIJINI ARUSHA,CHANJO KUPIGA HODI NYUMBA KWA NYUMBA.

    WATOTO 93,218 KUPATIWA CHANJO JIJINI ARUSHA,CHANJO KUPIGA HODI NYUMBA KWA NYUMBA.

    0
    By arushatv on September 1, 2022 Habari, Health

    Na Geofrey Stephen Arusha .

    Mkuu wa wilaya ya Arusha,Said Mtanda leo Septemba Mosi amezindua zoezi la chanjo ya polio ya matone kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano huku akisisitiza kuwa chanjo hiyo ni salama na haina madhara yoyote kwa binadamu.

    Pia amesisitiza ya kwamba zoezi hilo litadumu kwa siku nne hadi Septemba nne mwaka huu na kuongeza kuwa chanjo hiyo itawafikia hata wale walioko majumbani.

    Akizungumza wakati wa kuzindua zoezi hilo katika kituo cha afya cha Levolosi Mtanda alisema kuwa kila mzazi mwenye mtoto aliye chini ya umri wa miaka mitano ana wajibu wa kumpeleka mtoto wake akapatiwe chanjo kwa kuwa ni haki ya msingi.

    Hatahivyo,Mtanda amebainisha kwamba matarajio yake wilaya ya Arusha itaongoza katika zoezi hilo na kuwataka waratibu wa chanjo kuwapokea watoto wanaotoka katika wilaya za jirani.

    “Mnaoratibu zoezi la Chanjo  hakikisheni mnawalipa ujira wao wahamasishaji wa chanjo kabla jasho lao halijakauka “amesema Mtanda na kuibua shangwe kwa wahamasishaji wa zoezi hilo

    Naye kaimu mganga mkuu wa halmashauri ya jiji la Arusha,Dk Baraka Mundhe amesema kuwa katika kutekeleza kampeni hiyo jiji limepanga kuwafikia watoto 93,218 walio chini ya umri wa miaka mitano ili kuwakinga na ugonjwa wa Polio.

    Dk Mundhe amesema kwa siku wanatarajia kuchanja watoto 23,218 ambapo chanjo hiyo itatolewa katika vituo 64 vya huduma za pamoja ,mkoba na nyumba kwa nyumba katika maeneo ambayo hayana vituo.

    “Halmashauri ya jiji ilipokea jumla ya dozi 90,000 katika mgawo wa kwanza ambazo zimeshasambazwa katika vituo vya kutolea huduma “amesema Dk Mundhe.

    Mganga mkuu wa mkoa wa Arusha,Dk Slyvia Mamkwe amesema kuwa ugonjwa wa polio unapelekea ulemavu wa viungo na hata kifo na kuwataka wazazi kuhakikisha wanawapeleka watoti wao kwenye vituo vya afya na zahanati kupatiwa chanjo.

    Dk Mamkwe amesema kuwa mkoa wa Arusha unajivunia kwa kufanya vizuri katika zoezi la awamu ya pili la chanjo hiyo na kusisitiza kuwa awamu hii wamepanga kufikia asilimia 100.

    Mwisho.

    Post Views: 195
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleWAZIRI BASHUNGWA ALIKOROGA WADAU WA USAFIRI WAMVAA VIKALI ! MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV
    Next Article DC MTANDA WARATIBU WA ZOEZI LA CHANJO WALIPWE UJIRA WAO KABLA JASHO ALIJAKAUKA!

    Related Posts

    SERIKALI YAFUNGIA MGODI WA GEM AND ROCK VENTURE ULIOKO MIRERANI

    March 20, 2023

    TRA CHUNYA KUSAMBAZA ELIMU YA MLIPA KODI KWA WACHIMBAJI WA DHAHABU.

    March 16, 2023

    Wizara ya Madini imefanikiwa kutaifisha madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 4 yenye thamani ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture

    March 16, 2023

    DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

    March 16, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.