Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Makala»Serikali imeshauriwa kuwekeza nguvu kwa vijana hususani wajasiriamali wadogo wanaokuwa ili kuongeza Kasi ya viwanda nchini

    Serikali imeshauriwa kuwekeza nguvu kwa vijana hususani wajasiriamali wadogo wanaokuwa ili kuongeza Kasi ya viwanda nchini

    0
    By arushatv on September 14, 2022 Makala

    Na Pamela Mollel,Arusha

    Serikali imeshauriwa kuwekeza nguvu kwa vijana hususani wajasiriamali wadogo wanaokuwa ili kuongeza Kasi ya viwanda nchini

    Kwa Sasa Kuna uwekezaji pamoja na mafunzo mbalimbali ambayo yanatolewa na SIDO ingawaje uhitaji bado ni kubwa sana.

     

    Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa kampuni ya Bilsarm Investment Ali Babu wakati akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuhutimisha mafunzo ya mradi wa uanagenzi ambao ulikuwa unasimamiwa na SIDO

    Alisema kuwa kwa Sasa uwekezaji ambao unafanywa umeweza kuzaa matunda makubwa na matunda hayo yanatakiwa yaweze kuifukia jamii hususani vijijini

    Alisema kuwa endapo kama vijana wataweza kuwezeshwa kuanzia kwenye ngazi ya mafunzo wataweza kumiliki viwanda hivyo kuchochea ajira mpya kuzaliwa

    “Fursa zipo nyingi sana lakini wakat mwingine namna ya kuzifuata fursa hizo inakuwa ngumu hivyo kama uwekezaji utakuwa kwa kiwango kikubwa utaweza kufanya fursa nyingi”aliongeza

    Katika hatua nyingine aliwataka nao vijana ambao wamefanikiwa kupatiwa mafunzo pamoja na fursa mbalimbali kuhakikisha kuwa wanazitumia fursa hizo ipasavyo sanjari na kubuni ajira mpya kila mara.

    Akiongelea uwekezaji ambao ameufanya katika kiwanda Cha Bilsarm,alisema kuwa wao kama wadau wa kilimo wanajishugulisha na masuala mbalimbali ya kilimo

    Alisema kuwa uwekezaji wake umeweza kuzaa ajira nyingi kwa kuwa wanachakata nafaka mbalimbali

    “Sisi tunasambaza unga wa Dona,sembe,alizeti kwa kiwango kikubwa na kweli tunashukuru sana kwa kuwa mamlaka husika zimeweza kutuamini na Mimi niseme hii ni fursa kwa kuwa bidhaa zetu hizi tunaweza kuzisambaza hadi nje ya nchi”alisema

    Alihitimisha kwa kuwataka watanzania kujijengea utamaduni wa kupenda bidhaa za ndani ambapo kama wataunga mkono jitiada hizo basi wamiliki wa viwanda wataongezeka

    Post Views: 37
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleRUTO NCHI ZA AFRIKA WAIGE KENYA KWA UCHAGUZI WA DEMOKRASIA ! MAGAZETI YA LEO ARUSHA24TV
    Next Article MAUWAJI YATIKISA , MWALIMU AUA MKE KISA WIVU ,MAGAZETI YA LEO ARUSHA24TV

    Related Posts

    ASKOFU MASANGWA AKOSHWA NA MCHUNGAJI ALIYETUMIKIA KANISA KWA MIAKA34 AMEACHA ALAMA KUBWA

    February 26, 2023

    MZEE MOLLEL AZIKWA KIJIJINI KWAKE WANANCHI WAMWAGA MACHOZI WAZMIA WAKIAGA MWILI WAKE

    February 7, 2023

    WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezindua zoezi la ugawaji wa vishikwambi 293400 Kwa walimu wote nchini

    November 5, 2022

    PROFESA KIKULA AAINISHA MIKAKATI YA TUME YA MADINI KWENYE UBORESHAJI WA SEKTA YA MADINI

    October 13, 2022

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.