Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Siasa»RUTO RAIS WA KENYA ! MASKINI RAILA ASHINDWA TENA MAHAKAMANI RASMI KURUDI NYUMBANI

    RUTO RAIS WA KENYA ! MASKINI RAILA ASHINDWA TENA MAHAKAMANI RASMI KURUDI NYUMBANI

    0
    By arushatv on September 5, 2022 Siasa

    Mahakama ya juu imeidhinisha Uchaguzi wa William Ruto kuwa rais mteule wa Kenya baada ya kesi iliowasilishwa na mpinzani wake mkuu katika uchaguzi huo Raila Odinga kukosa ushahidi wa kutosha.

    Wakitoa uamuzi wao wa pamoja, majaji hao walioongozwa na jaji mkuu Martha Koome walisema kwamba ushahidi uliotolewa na mlalamishi Raila Odinga ulikuwa umejaa uvumi na porojo.

    Akiangazia maswala tisa ya kesi hiyo, Jaji Martha Koome amesema kuwa mshindi wa uchaguzi huo William Ruto alifanikiwa kupita kikwazo cha kura asilimia 50 na moja ya kikatiba.

    Akitangaza matokeo hayo , mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati, alimtangaza Dkt Ruto kuwa Rais mteule baada ya kupata kura milioni 7,176,141 (asilimia 50.49) dhidi ya milioni 6,942,930 za Bw Odinga (asilimia 48.85) )Prof George Wajackoyah wa Roots Party alifanikiwa kura 61,969 (asilimia 0.44) huku David Mwaure Waihiga wa Agano Party akiibuka wa nne kwa kura 31,987 (asilimia 0.23).

    lakini akitoa uamuzi huo jaji mkuu Martha Koome alisema kwamba kura zilizokataliwa haziwezi kujumlishwa katika hesabu ya kumtafuta aliyeibuka mshindi.

    Bi Koome alisema kwamba mbinu iliotumika na tume ya uchaguzi kupata asilimia 64.4 ya wapiga kura ilikuwa sahihi.

    Post Views: 94
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleKESI YA URAIS KENYA UAMUZI LEO ! NI RUTO AU RAILA KUONGIA IKULU MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV
    Next Article SAKATA LA TOZO LATINGA MAHAKAMANI ! MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA24TV

    Related Posts

    MRITHI WA MREMA WA TLP KUPATIKANA KESHO UCHAGUZI WAPAMBA MOTO

    March 5, 2023

    CCM NA SERIKALI SAMBAMBA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI IKUNGI

    January 17, 2023

    JUMUIYA YA WAZAZI TAIFA YAMPONGEZA RAIS SAMIA TAMKO LA MIKUTANO YA HADHARA

    January 4, 2023

    MIKUTANO YA HADHARA RUKSA IGP WAPE VIBALI MUDA WOWOTE

    January 3, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.