Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»NABII MKUU DKT GEORDAVIE KUWASHIKA MKONO WAFANYABIASHARA ZAIDI YA 5,000 SOKO LA SAMUNGE JIJINI ARUSHA.

    NABII MKUU DKT GEORDAVIE KUWASHIKA MKONO WAFANYABIASHARA ZAIDI YA 5,000 SOKO LA SAMUNGE JIJINI ARUSHA.

    0
    By arushatv on September 21, 2022 Habari

    Moses Mashalla,

    Zaidi ya wafanyabiashara 5,000 wanaofanya biashara katika soko la Samunge jijini Arusha wanataraji kupatiwa mitaji ya kuendesha biashara zao na mhubiri maarufu nchini Nabii Mkuu Dkt GeorDavie.

    Mbali na kupatiwa mitaji hiyo pia mhubiri huyo anataraji kutoa msaada wa kukarabati miundombinu ya malango ya kuingilia ndani ya soko hilo kama njia mojawapo ya kusaidia jamii.

    Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko la Samunge,Joram Miraji amesema kuwa uongozi wa soko hilo hivi karibuni ulimwandikia barua ya maombi ya kuwasaidia mitaji wafanyabiashara ndani ya soko hilo pamoja na kusaidia kukarabati miundombinu ambapo ombi lao limekubaliwa.

    Miraji amesema kuwa baadhi ya wafanyabiashara ndani ya soko hilo hawana mitaji kufuatia soko hilo kuungua mwaka 2019 na kuteketeza mali zao.

    Mwenyekiti huyo amesema kuwa wafanyabiashara wengi ndani ya soko hilo wanaishi kwa mateso kufuatia kudaiwa mikopo na baadhi ya benki nchini hali ambayo imepelekea kero na usumbufu kwa uongozi wao.

    Miraji amesisitiza kuwa hatua ya kumuandikia barua Nabii Mkuu Dkt GeorDavie imekuja baada ya kuona anasaidia makundi mbalimbali kwenye jamii hivyo na wao waliona wamuandikie barua na tayari wameshapatiwa majibu kuwa atawatembelea.

    Naye mweka hazina wa soko hilo ,Amos Julius amesema kwamba soko lao linakabiliwa na changamoto ya miundombinu hususani malango ya kuingilia na kupelekea baadhi ya wafanyabiashara kuibiwa bidhaa zao.

    “Soko liko wazi sana na hii imepelekea baadhi ya wezi kupenya na kuchukua bidhaa za wafanyabiashara hivyo tunamuomba Nabii Mkuu Dkt GeorDavie atusaidie katika hili “amesema Julius

    Mfanyabiashara Upendo Remy amesema kuwa pindi moto ulipounguza soko hilo alijikuta akipata hasara ya sh 500,000 na sasa anaishi kwa mikopo.

    Naye Agripina Kawalla amesema kuwa wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mitaji ya kuendesha biashara zao na endapo Nabii Mkuu Dkt GeorDavie akiwashika mkono watainuka kiuchumi.

    Hivi karibuni akiwa katika ibada katika huduma yake ya Ngurumo ya Upako Nabii Mkuu Dkt GeorDavie alitoa kauli ya kufanya ziara ya kutembelea soko la Samunge na kuwasaidia changamoto mbalimbali kama mitaji wafanyabiashara waliopo ndani ya soko hilo.

    Mwisho…..

    Post Views: 120
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleCHADEMA YATANGAZA MIKUTANO YA ADHARA NCHI NZIMA ! MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV .
    Next Article A.TO.Z KUKAMILISHA MTAMBO WA KUCHAKATA MAJI TAKA

    Related Posts

    SERIKALI YAFUNGIA MGODI WA GEM AND ROCK VENTURE ULIOKO MIRERANI

    March 20, 2023

    TRA CHUNYA KUSAMBAZA ELIMU YA MLIPA KODI KWA WACHIMBAJI WA DHAHABU.

    March 16, 2023

    Wizara ya Madini imefanikiwa kutaifisha madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 4 yenye thamani ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture

    March 16, 2023

    DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

    March 16, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.