Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»LHRC watoa msaada wa kisheria Singida mamia wajitokeza

    LHRC watoa msaada wa kisheria Singida mamia wajitokeza

    0
    By arushatv on September 8, 2022 Habari

    Na Mwandishi wa A24Tv Singida

    Arusha.Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu(LHRC) kimeanza kutoa bure ushauri wa kisheria kwa wananchi wa mkoa wa Singida.

    Akizungumza na waandishi,Wakili Hamis Mayombo alisema zoezi hilo ambalo limeanza jumatatu wiki hii litakuwa la wiki moja.

    Wakili Mayombo amesema hadi Sasa mashauri mengi ambayo wamekuwa wakipokea ni migogoro ya ardhu,masuala ya mirathi na utawala bora, baadhi yatafikishwa mahakamani na mengine kupatiwa suluhu.

    Wakili Mayombo ambaye ni Mkuu wa LHRC Ofisi ya Arusha,alisema mashauri ya ndoa yanatokana na migogoro ya kifamilia huku migogoro ya ardhi ikitokana na uvamizi wa ardhi.

    Wakili w Fides Mwenda alisema baadhi ya mashauri ambayo wamepokea tayari yamefikishwa mahakamani na mengine bado.

    “lakini pia kuna malalamiko ya viongozi kukiuka misingi ya utawala bora hivyo wamelalamikiwa”alisema

    Mmoja wa Wananchi hao, Michael Itembe alisema anataka msaada wa kisheria kusaidiwa kupata shamba lake ambalo limevamiwa na ndugu zake na kulima bila idhini yake.

    “naomba LHRC isaidie kisitishwa kilimwa katika ardhi yangu hadi kesi ya msingi imalizike”alisema

    LHRC itatoa huduma za kisheria kwa wiki moja mkoani Singida.

    Jumanne Issa alieleza kuvamia ardhi yake na tayari shauri limefishwa mahakama I lakini hata hivyo bado suluhu haijapatikana.

    Rehema Peter mkazi wilaya ya Ikungi alieleza kusumbuliwa na ndugu wa marehemu mume wake katika suala la mirathi kwani wanataka kunyang’a ya Mali zake.

    mwisho

    Post Views: 68
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleLISU KUREJEA TANZANIA MIAKA MITANO IMEPITA TOKA AONDOKE ! MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA24TV
    Next Article TOZO KAA LA MOTO YATIKISA VIKAO VYA CCM ! MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA24TV

    Related Posts

    Tanzania na India kuendeleza Uhusiano wa Kibiashara na Uwekezaji

    March 27, 2023

    TANZANIA YAKABILIWA NA UHABA WA MABAHARIA VIJANA.

    March 27, 2023

    Marcas Ajitosa kuwania U NEC Arusha

    March 25, 2023

    VIKUNDI 47 KUPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI MOITA MONDULI

    March 24, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.