Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»Maarifa ya asili yasaidia uhifadhi wa misitu na vyanzo vya Maji Loliondo.

    Maarifa ya asili yasaidia uhifadhi wa misitu na vyanzo vya Maji Loliondo.

    0
    By arushatv on September 11, 2022 Habari

    Na Mwandishi wa A24Tv . Loliondo

    Arusha. Matumizi ya maarifa ya asili katika uhifadhi wa misitu, vyanzo vya maji na Mazingira umesaidia jamii ya wafugaji Kata ya Enguserosambu kutoathirika na mabadiliko ya tabia nchi.

    Wakizungumza na waandishi wa habari waliofika katika Kata hiyo, ,kupitia mradi wa uhifadhi Mazingira kwa maarifa asilia ambao unatekelezwa na taasisi ya Usaidizi wa jamii za Pembezoni (MAIPAC) kwa kishirikiana na taasisi ya CILAO katika mradi unaodhaminiwa na shirika la maendeleo la umoja wa mataifa(UNDP) kupitia program ya miradi midogo na kuratibiwa na Jumuiko la maliasili Tanzania (TNRF) baadhi ya viongozi wa Mila na serikali wameeleza matumizi ya maarifa ya asili yamekuwa na ufanisi mkubwa.

    viongozi wa hao wamila na serikali katika Kata ya Enguserosambu,walieleza kuwa na sheria kali imesababisha, mazingira na kufanya kata hiyo, kuwa na msitu mkubwa wa asili wenye hekta 14,700.

    Kiongozi wa Mila Parmitoro Pumbun alisema wamekuwa na sheria ya Mila kutoza faini ya Ndama jike, kulaaniwa ama kunyang’anywa mke kwa ambao watabainika kukata Miti ama kuharibu Mazingira.

    Laigwanani Pumban alisema faini hizo, zimesababisha Kata yao kuwa ya mfano katika utunzwaji wa mazingira kwa kutumia maarifa ya asili.

    Ngarashe Kipurda akionesha majani ya mti wa katika msibu wa Enguserosambu ambayo ni dawa ya mafua

    Katibu wa bodi ya msitu wa Enguserosambu, Marko Tarash alisema msitu wao umekuwa na faida kubwa kwa jamii kwani, wana uhakika kupata malisho ya mifugo mwaka mzima,kupata dawa za asili,matunda,maji na Kuni za kupikia.

    Tarash alisema msitu huo unaundwa na vijiji vinne ambavyo ni Enguserosambu,Ng’arwa,Orkiu na Naan.

    Wananchi wa Kata ya Enguserosambu sambu tarafa ya Loliondo wilaya ya Ngorongoro wakionesha manufaa ya maarifa ya Asili

    Afisa Mtendaji Kijiji cha Enguserosambu Duni Mollel alisema uwepo Sheria za Mila umesaidia sana uhifadhi kwani Wananchi wanaziheshimu zaidi.

    “Ingawa tuna sheria ndogondogo za serikali kuhifadhi misitu na vyanzo vya maji lakini Sheria za Mila ndizo zinaogopwa zaidi na Wananchi wa huku”alisema.

    Mwalimu Edward Sasi wa shule ya msingi Enguserosambu alisema licha ya kuwepo elimu ya kisayansi lakini nao wao katika shule wamekuwa wakisisitiza wanafunzi kuzingatia elimu ya asili katika uhifadhi.

    “Vijana wanajua misitu ndio maisha Yao kwani wanategemea mifugo Sasa ikiathirika na kukosa malisho na maji wao ndio wanapata shida Sasa wanajituma kutunza Mazingira na vyanzo vya maji”alisema.

    Mwanafuzi Regina Zakayo alisema utunzwaji wa misitu umekuwa na faida kubwa hata kwao kwani kwenye msitu huo pia wanapata maji na dawa sa asili ambazo wanaotumia kutibu magonjwa mbalimbali.

     

    Mwisho

    Post Views: 101
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleYANGA,SIMBA ZANGA,RA KIMATAIFA MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA24TV
    Next Article MCHAKATO WA BIMA YA AFYA KWA WOTE KUPIGA HODI BUNGENI ! MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA24TV

    Related Posts

    Kamati yapitisha makadirio ya matumizi na maendeleo 2023/2024 kwa Wizara Uwekezaji Viwanda na Biashara.

    March 23, 2023

    MWANDISHI WA HABARI MAARUFU ALLAN ISACK AITAKA NAFASI YA MNEC

    March 23, 2023

    Vyombo vya Dola na wanasheria kushirikiana kutokomeza ujangili Babati

    March 22, 2023

    JIJI LA ARUSHA LATOA MIKOPO YA SHILINGI BILION 2.6 KWA VIJANA WENYE MAITAJI MAALUM NA WANAWEKE

    March 22, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.