Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»TEMDO YAJA USANIFU WA MASHINE ZA KISASA YAWAKARIBISHA WAEKEZAJI KATIKA BANDA LAO NANE NANE ARUSHA

    TEMDO YAJA USANIFU WA MASHINE ZA KISASA YAWAKARIBISHA WAEKEZAJI KATIKA BANDA LAO NANE NANE ARUSHA

    0
    By arushatv on August 4, 2022 Habari

    Na Geofrey Stephen Arusha

    Taasisi ya uhandisi na usanifu mitambo nchini (TEMDO) imebuni mtambo mpya wa kisasa wa kuchakata mafuta ya alizeti ambayo yatasafishwa katika ubora kwa kiwango cha juu kwa  ajili ya matumizi ya binadamu.

    Taasisi hiyo imeutambulisha mtambo huo kwa mara ya kwanza katika maonyesho ya sikukuu za wakulima nchini (Nane Nane) yanayoendelea katika viwanja vya Nanenane eneo la Njiro jijini Arusha.

    Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa kitengo cha mawasiliano na masoko katika taasisi hiyo,dkt Sigisbert Mmasi alisema kwamba mtambo huo mbali na kuchakata mafuta ya alizeti lakini utayasafisha mafuta hayo na kisha kutawekea virutubisho.

    Alisema kwamba mtambo huo utasaidia kusafisha mafuta ghafi ya alizeti ambayo yana athari kwa afya ya binadamu  na kuyasafisha katika ubora huku akiwataka wakulima kuwekeza katika mtambo huo kwa manufaa ya biashara zao.

    Mbali na mtambo huo mitambo mingine iliyobumiwa na taasisi hiyo ni ,mtambo wa kuchakata Sukari,mtambo wa kukamua mafuta ya Parachichi,Kiteketezi xha kuchoma taka za hospitalini ,vifaa tiba kama vitanda ,stand ya drip na jokofu la kuhifadhia maiti.

    “Tumekuja nanenane kuwaonyesha wamulima huu mtambo wa kuchakata mafuta ya alizeti hivyo mtambo huu utawasaidia wakulima nawaomba wawekeze kwenye huu mtambo”alisema Mmasi .

    Awali mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango alizitaka taasisi za kilimo  kubuni zana mbalimbali zitakazowasaidia wakulima katika shughuli zao na aliipongeza taaisisi ya Temdo kwa ubunifu wa mitambo mbalimbali itakayosaidia maendeleo ya kilimo, mifugo na uvuvi nchini .

    Aliyasema hayo jijini Arusha  ,kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha wakati akifungua maonyesho ya kilimo na mifugo nanenane yenye kauli mbiu ya”agenda 10/30 kilimo ni biashara ,shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo,mifugo na uvuvi”.

    Alisema kuwa,  maonyesho hayo yanatarajiwa   kuchangia ukuaji wa mabadiliko kwa wakulima kutoka maeneo mbalimbali endapo elimu ya kutosha itatolewa  na kuenea kwa elimu kwa jamii inayowazunguka juu ya killimo na ufugaji wa kisasa .

    Aidha aliwataka watalaamu wa kilimo nchini kuendelea kutoa elimu ya kutosha kwa wakulima na wafugaji ili walime na kufuga kisasa na kuepukana  na kuondokana na zana za zamani na hatimaye kuweza kubadilisha maisha yao.

    Naye Mkuu wa wilaya ya Kiteto ,Mbaraka Alhaji Yusuph alisema kuwa,maonyesho hayo yameshirikisha waonyeshaji 200 kutoka Taasisi mbalimbali licha ya taarifa kuchelewa juu ya uwepo wa maonyesho,lakini mwitikio bado ni mkubwa sana.

    Ends..

    Post Views: 305
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleUTATA WAIBUKA KUHUSU UJENZI WA JENGO LA BIASHARA ARUSHA,JIJI WAPIGA “STOP”, KIGOGO CCM AHUSISHWA
    Next Article BOSS ADAIWA KUBAKA OFISINI KWAKE MTUMISHI MAGAZETI YA LEO A24TV

    Related Posts

    Kamati yapitisha makadirio ya matumizi na maendeleo 2023/2024 kwa Wizara Uwekezaji Viwanda na Biashara.

    March 23, 2023

    MWANDISHI WA HABARI MAARUFU ALLAN ISACK AITAKA NAFASI YA MNEC

    March 23, 2023

    Vyombo vya Dola na wanasheria kushirikiana kutokomeza ujangili Babati

    March 22, 2023

    JIJI LA ARUSHA LATOA MIKOPO YA SHILINGI BILION 2.6 KWA VIJANA WENYE MAITAJI MAALUM NA WANAWEKE

    March 22, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.