Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»OMAN YAVUTIWA KUWEKEZA TANZANIA

    OMAN YAVUTIWA KUWEKEZA TANZANIA

    0
    By arushatv on August 10, 2022 Habari

    Na Mwandishi wa A24Tv .

    Serikali ya Oman imevutiwa kuwekeza katika madini ya viwandani na madini ya ujenzi nchini.

    Kauli hiyo, ameitoa Balozi wa Oman nchini Tanzania Said All-Shidham baada ya kukutana na Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko katika Ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.

    Balozi Shidham amesema nchi ya Oman imevutiwa kuwekeza kutokana na hali ya utulivu uliyopo nchini, amani, na mazingira wezeshi kwenye Sekta ya Madini chini ya Uongozi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

    Kwa upande wake, Dkt. Biteko amesema milango ya Wizara ya Madini kwa wawekezaji iko wazi na kuwataka wale wote wenye nia ya kuwekeza kwenye Sekta ya Madini nchini Tanzania wafike Wizarani hapo.

    Aidha, Dkt. Biteko amesema Wizara ya Madini inawahitaji wawekezaji kuliko wawekezaji wanavyoihitaji Wizara hiyo ambapo amewaomba waje nchini kuwekeza kwenye sekta hiyo.

    Pia, Dkt. Biteko amekutana na kuzungumza na Kampuni ya uchimbaji wa madini ya almasi ya Williamson Diamond Limited (DWL) kwa lengo la kupata mrejesho wa kikao kilichofanyika awali.baada ya kukutana na Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko katika Ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.

    Balozi… amesema nchi ya Oman imevutiwa kuwekeza kutokana na hali ya utulivu uliyopo nchini, amani, na mazingira wezeshi kwenye Sekta ya Madini chini ya Uongozi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

    Kwa upande wake, Dkt. Biteko amesema milango ya Wizara ya Madini kwa wawekezaji iko wazi na kuwataka wale wote wenye nia ya kuwekeza kwenye Sekta ya Madini nchini Tanzania wafike Wizarani hapo.

    Aidha, Dkt. Biteko amesema Wizara ya Madini inawahitaji wawekezaji kuliko wawekezaji wanavyoihitaji Wizara hiyo ambapo amewaomba waje nchini kuwekeza kwenye sekta hiyo.

    Pia, Dkt. Biteko amekutana na kuzungumza na Kampuni ya uchimbaji wa madini ya almasi ya Williamson Diamond Limited (DWL) kwa lengo la kupata mrejesho wa kikao kilichofanyika awali.

    Post Views: 312
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleRAIS SAMIA AWALILIA WALIO POTEZA MAISHA KATIKA AJALI ! MAGAZETI YA LEO A24TV
    Next Article STAMICO KUZINDUA MATUMIZI MKAA MBADALA WA KUPIKIA IKIADHIMISHA MIAKA 50

    Related Posts

    SERIKALI YAFUNGIA MGODI WA GEM AND ROCK VENTURE ULIOKO MIRERANI

    March 20, 2023

    TRA CHUNYA KUSAMBAZA ELIMU YA MLIPA KODI KWA WACHIMBAJI WA DHAHABU.

    March 16, 2023

    Wizara ya Madini imefanikiwa kutaifisha madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 4 yenye thamani ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture

    March 16, 2023

    DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

    March 16, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.