Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»Mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanga imefanikiwa kuvuka lengo la kuhudumia jumla ya tani 867,00 baada ya uwekezaji mkubwa

    Mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanga imefanikiwa kuvuka lengo la kuhudumia jumla ya tani 867,00 baada ya uwekezaji mkubwa

    0
    By arushatv on August 16, 2022 Habari

    Na Geofrey Stephen .Arusha

    Mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanga imefanikiwa kuvuka lengo la kuhudumia jumla ya tani 867,00 ikiwa ni Matokeo ya awali mara baada ya uwekezaji mkubwa wa bandari hiyo

    Akiongea na waandishi wa habari mapema Leo jijini hapa Msemaji wa bandari hiyo Peter milanzi alisema kuwa uboreshaji huo ulianza toka mwaka 2019.

    Milanzi alisema kuwa katika mamlaka hiyo tangu kujengwa kwake,Bandari ya Tanga ilikuwa inahudumia shehena katika kina kirefu Cha maji (Stream Operation)eneo la umbali wa kilomita 1.7kutoka gatini kwa sababu ya changamoto ya kina kifupichq maji eneo la gati amabpi kina Cha maji kilikuwa ni mita 3

    Aliongeza kuwa hali hiyo ilikuwa inafanya melu kubwa kushindwa kufika gatini,ambapo kutokana na changamoto hiyo serikali kupitia mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania iliamua kufanya uwekezaji mkubwa ili kutatua changamoto hiyo kwa lengo la kuhudumia meli nyingi na shehena kubwa zaidi.

    “Mamlaka husika iliona changamoto hiyo Serikali iliamua kutenga fedha jumla ya Bilioni 429.1 ili kutekeleza mradi mkubwa na WA kimataifa katika bandari ya Tanga na mradi huo wa maboresho ya bandari iliweza kutekelezwa katika awamu mbili”alisema

    Milanzi aliendelea kwa kusema kuwa katika awamu hizo Agosti 3 TPA iliingia mkataba wa miezi 12 na kampuni ya china Harbour Engineering company (CHEC)limited na mhandisi mshauri wa mradi ni kampuni ya NIRAS kutoka denrmak ikishirikiana na kampuni ya kizawa ijulikanayo kwa jina la ANOVA

    “Awamu hiyo ya kwanza ya mradi ilihusisha uchimbaji wa kina Cha maji kwenye mlango wa kuingilia meli (enterance channel)na sehemu yakugeuzia meli (turning basin)kutoka mita 3 hadi mita 13 pamoja na ununuzi wa mitambo ya bandari (operation equipment)kwa gharama ya shilingi 172.

    “Awamu ya pili kumfuatilia utekelezaji wenye mafanikio wa mradi wa utekelezaji wenye mafanikio wa mradi wa maboresho ya bandari ya Tanga na utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 61,mkandarasi tayari ameshakabidhi kipande chenye urefu wa mita 200 hali hiyo imewezesha Bandari ya Tanga kuanza kupokea melu na kuhudumia meli na kuhudumia meli gatini zisizozidi mita 200 kama ilivyofanyika katika bandari ya Dar es salaam.

    Mbali na hayo aliwataka wafanyabiashara wa Kanda ya kaskazini kuhakikisha kuwa wanatumia vyema bandari hiyo kwa kuwa mpaka Sasa wameshaiboresha kwenye viwango vya ngazi ya kimataifa

    Alihitimisha kwa kusema kuwa wameshafanya mafunzo maalumu kwa wahudumu sanjari na kuwapa mbinu mbalimbali za kibiashara za kimataifa.

    Mwisho

    Post Views: 117
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleNI RUTO RAIS WA 5 , ODINGA APINGA MATOKEO ! MAGAZETI YA LEO A24TV
    Next Article Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga Ametaka Ujenzi wa Mabweni Kukamilika Mapema

    Related Posts

    Tanzania na India kuendeleza Uhusiano wa Kibiashara na Uwekezaji

    March 27, 2023

    TANZANIA YAKABILIWA NA UHABA WA MABAHARIA VIJANA.

    March 27, 2023

    Marcas Ajitosa kuwania U NEC Arusha

    March 25, 2023

    VIKUNDI 47 KUPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI MOITA MONDULI

    March 24, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.