Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»MAANDAMANO YA KUHAMASISHA SENSA ARUSHA YAFANA ,TAASISI YA KIDINI YA TWARIQATUL QADIRIYA JAILANIYA ARRAZAQIYA YAPONGEZWA

    MAANDAMANO YA KUHAMASISHA SENSA ARUSHA YAFANA ,TAASISI YA KIDINI YA TWARIQATUL QADIRIYA JAILANIYA ARRAZAQIYA YAPONGEZWA

    0
    By arushatv on August 21, 2022 Habari

    Na Joseph Ngilisho, ARUSHA

    MAMIA ya wakazi wa jiji la Arusha wamejitokeza kwa wingi kushiriki maandamano makubwa ya kuhamasisha zoezi la sensa ya watu na makazi yaliyoandaliwa naTaasisi ya dini ya kiislamu ya Twarika Qadiriya mkoani Arusha ambapo wananchi hao walisema wapo tayari kuhesabiwa.

    maandamano ya sensa na makazi jijini Arusha

    Akiongea mara baada ya kupokea ujumbe wa maandamano hayo ,kamishna wa ardhi Mkoa wa Arusha,Essay Mwakatumbula aliwataka wananchi hao kuwa mabalozi wazuri wa kuhamasisha zoezi la Sensa ili kila mtu ashiriki kikamilifu zoezi hilo.

    Aidha aliwataka wakazi wa jiji la Arusha kutoa ushirikiano wa dhati kwa makarani wa Sensa ikiwemo kutowaficha wenye ulemavu ili kuiwezesha serikali kuwatambua ili kuwapatia fursa mbalimbali.

    Mwakatumbula ambaye alimwakilisha waziri wa Ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi, Angeline Mabula, alisema ofisi yake itaendelea kushirikiana na taasisi hiyo ya dini katika kufanikisha zoezi la serikali la uhesabuji wa watu na makazi lenye lengo la kuirahisishia serikali katika kupanga mipango ya maendeleo.

    Katika hatua nyingine Mwakatumbula alisema kuwa waziri Mabula amepokea ombi la taasisi ya Twarika kuhusu mpango wake wa kupata eneo lenye ukubwa wa ekari 10 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya mama na mtoto,ambapo waziri aliahidi kuchangia .

    Kwa upande wake katibu wa taasisi hiyo ya kidini ya Twarika, mkoani hapa,Sheikh Haruna Husein alisema kuwa lengo la maandamano hayo ni kuhamasisha zoezi la Sensa ya watu na makazi inayotarajia kufanyika nchini nzima Agosti 23,mwaka huu.

    Alisema maandamano hayo ambayo yalishirikisha vikundi mbalimbali vya maendeleo,wanasiasa, waendesha pikipiki,wazee wa ukoo na wananchi yalizunguka katika mitaaa mbalimbali ya jiji la Arusha huku yakichagizwa na vikundi vya ngoma na sarakasi .

    “Tunawapongeza sana wananchi waliohamasika kushiriki maandamano haya ya kuhamasisha zoezi la Sensa, sisi kama taasisi ya dini tumefarijika sana kuona wananchi wameielewa serikali yao”alisema.

    Wananchi walioshiriki maandamano hayo waliipongeza taasisi hiyo ya kidini kwa kuwa mstari wa mbele kuhamasisha mara kwa mara watu kujitoleza kuhesabiwa na walidai kuwa wapo tayari kuhesabiwa .

    Ends..

    Post Views: 111
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleRAIS SAMIA ASISITIZA SENSA TAREHE 23 MAPUMZIKO ! MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV.
    Next Article SIMANZI KILA KONA WATANZANIA WAMLILIA MREMA ! MAGAZETI YA LEO ARUSHA24TV

    Related Posts

    SERIKALI YAFUNGIA MGODI WA GEM AND ROCK VENTURE ULIOKO MIRERANI

    March 20, 2023

    TRA CHUNYA KUSAMBAZA ELIMU YA MLIPA KODI KWA WACHIMBAJI WA DHAHABU.

    March 16, 2023

    Wizara ya Madini imefanikiwa kutaifisha madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 4 yenye thamani ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture

    March 16, 2023

    DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

    March 16, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.