Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»DC MTANDA MARUFUKU KUVAA SARE ZA VYAMA WAKATI ZOEZI LA SENSA

    DC MTANDA MARUFUKU KUVAA SARE ZA VYAMA WAKATI ZOEZI LA SENSA

    0
    By arushatv on August 22, 2022 Habari

    Na Geofrey Stephen Arusha

    Wakati zoezi la Sensa ya watu na makazi likitarajiwa kuanza hapo kesho,mkuu wa wilaya ya Arusha,Saidi Mtanda amepiga marufuku kwa makarani  na wote watakao ambatana  katika zoezi hilo, kutovaa mavazi yenye mlengo wa vyama vya siasa ili kuepusha kutia dosari zoezi hilo.

    Akiongea na waandishi wa habari mapema leo ofisini kwake,amesema kuwa maandalizi ya zoezi hilo wilayani humo yamekamilika ,na hatua ya kwanza ya dodoso la kuhesabu linatarajia kuanza saa 6.01 usiku kwa  makundi maalumu yakiwemo ya watoto wa mtaani na waliolala hotelini na nyumba za kulala wageni.

    Alisema kuwa zoezi la Sensa halina itikadi ya kisiasa ,kidini wala kikabila na kuwataka makarani wa Sensa kutodhubutu kuvaa vazi lolote linalotambulisha chama cha siasa.

    Mtanda alisema kuwa zoezi la sensa kimkoa litazinduliwa leo majira saa sita usiku na mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela katika makumbusho ya mnara wa Azimio la Arusha, ambapo pamoja na mambo mengine atafyatua fataki maalumu kama ishara ya uzinduzi.

    Alifafanua kuwa zoezi la uhesabuji watu litaanza mapema agosti 23 hadi agosti 28 na Agosti 28 makarani wa Sensa wakiwa wameambatana na  wenyeviti wa mitaa na watendaji wataendelea na dodoso la majengo hadi septemba 6 litakapofungwa rasimi zoezi hilo.

    Aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa makarani  wa Sensa ili kufanikisha zoezi hilo .

    Aidha amelitaka jeshi la polisi mkoani hapa,kuhakikisha linaimarisha ulinzi na usalama hasa katika uzinduzi wa zoezi hilo .

    Ends….

    Post Views: 188
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleSIMANZI KILA KONA WATANZANIA WAMLILIA MREMA ! MAGAZETI YA LEO ARUSHA24TV
    Next Article KIKWETE NA VIONGOZI WENGINE WAMLILIA MREMA ! MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV

    Related Posts

    Tanzania na India kuendeleza Uhusiano wa Kibiashara na Uwekezaji

    March 27, 2023

    TANZANIA YAKABILIWA NA UHABA WA MABAHARIA VIJANA.

    March 27, 2023

    Marcas Ajitosa kuwania U NEC Arusha

    March 25, 2023

    VIKUNDI 47 KUPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI MOITA MONDULI

    March 24, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.