Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuzindua onyesho la Sita la Swahili International Tourism Expo-S!TE 2022

    Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuzindua onyesho la Sita la Swahili International Tourism Expo-S!TE 2022

    0
    By arushatv on July 17, 2022 Habari

    Na Geofrey Stephen ARUSHA

    Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) inatarajia kuzindua onesho la Sita la Swahili International Tourism Expo-S!TE 2022 litakalohudhuliwa na waoneshaji na wanunuzi wa kimataifa zaidi ya 550 kutoka katika masoko ya utalii duniani ikiwa ni mwendelezo wa programu ya Royal  Tour hapa nchini.

    Akiongea na waandishi wa habari Mkoani Arusha,waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt Pindi Chana alisema kuwa onesho hilo litafanyika katika ukumbi wa mlimani City jijini Dar es salaam,oktoba 21 hadi 23 mwaka huu.

    Alisema onesho hilo litakuwa mahususi kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kuonesha bidhaa mbalimbali za utalii likiwa na lengo la kutangaza na kukuza utalii nchini.

    Alisema tangu kuanzishwa kwa SiTE mwaka 2014 ,kumekuwepo na mafanikio  makubwa ikiwemo ongezeko la waoneshaji na wanunuzi wa kimataifa ambapo mwaka 2014 hadi 2019 waoneshaji waliongezeka kutoka 40 hadi 170,huku wanunuzi wa Kimataifa wakifikia 333 kutoka 24

    “Baada ya dunia kukumbwa na athari za janga la ugonjwa wa UVICO-19 mwaka 2019, serikali ililazimika kusitisha onesho hilo kwa muda”alisema.


    Hata hivyo serikali ilichukua hatua mbalimbali zenye lengo la kuinusuru sekta hiyo ya utalii,na jitihada hizo zimewezesha kurejeshwa upya kwa onesho hilo.

    Waziri Chana alisema kuwa onesho hilo litawahusisha watangazaji wa bidhaa mbalimbali za utalii,jukwaa la uwekezaji,semina kuhusu masuala ya utalii, masoko pia mikutano ya wafanyabiashara wa bidhaa za Utalii.

    Alisema kuwa onesho la SiTE  litakwenda sambamba  na utekelezaji wa Sera ya Taifa ya utalii ya mwaka 1999 ,pamoja na mkakati wa mwaka 2020-2025 wa  kuitangaza Tanzania  Kimataifa kuhusu utalii.

    Alisema onesho  hilo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano awanu ya tatu (FYDP III 2021/22-2015/26 ambapo zao lanutalii wa mikutano limeainishwa kama zao la utalii la kimkakati kwa lengo la kufikia watalii milioni tano na kufikia mapato ya dola za kimarekani  bilioni 6 ifikapo 2025.

     

    Awali kaimu mkurugenzi  mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB,Felix John alisema kuwa bodi yake imeshakamilisha maandalizi yote ya onesho hilo na kuwataka wadau wachangamkie fursa hiyo.

    Aliongeza kwa kuwataka wadau wa utalii kutumia onesho hilo katika kuandaa  vyakula vya asili kwa sababu watakao hudulia watapenda kuona vyakula vya  tamaduni za kitanzania .

    Ends…

    Post Views: 516
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleUCHUMI UNAPAA NCHINI MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV
    Next Article LIPUMBA AMWAGIA SIFA RAIS SAMIA KWA UTAWALA BORA MAGAZETI YA LEO A24TV

    Related Posts

    Tanzania na India kuendeleza Uhusiano wa Kibiashara na Uwekezaji

    March 27, 2023

    TANZANIA YAKABILIWA NA UHABA WA MABAHARIA VIJANA.

    March 27, 2023

    Marcas Ajitosa kuwania U NEC Arusha

    March 25, 2023

    VIKUNDI 47 KUPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI MOITA MONDULI

    March 24, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.