Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Break News»WATAALAM WATEMBELEA SHULE YA CHIEF ALBART LUTHULI MOROGORO

    WATAALAM WATEMBELEA SHULE YA CHIEF ALBART LUTHULI MOROGORO

    0
    By arushatv on July 27, 2022 Break News

    Ujumbe wa wataalamu kutoka Wizara ya Elimumsingi ya Afrika Kusini umetembelea shule ya Msingi Chief Albert Luthuli iliyopo Mazimbu Mkoani Morogoro.

    Shule hii iko katika moja ya eneo waliloishi wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini wakati wa harakati za ukombozi wa nchi hiyo.

    Akiwa Shuleni hapo Mkuu wa Msafara huo, Enoch Rabotapi ambaye ni Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Elimu ya Ualimu nchini humo (Chief Director Teacher Development) ameahidi ushirikiano kati ya shule hiyo na baadhi ya shule zitakazobainishwa nchini Afrika Kusini kwa kubadilishana uzoefu na walimu.

    “Uhusiano wa nchi ya Tanzania na Afrika ya Kusini ni wa muda mrefu, na itakumbukwa mwaka 2018 Rais wetu wa Afrika Kusini akiwa nchini Tanzania aliahidi kutembelea shule hii. Na hivi juzi Mwezi huu wa Julai Waziri wetu wa Elimu ya Msingi nae alitoa ahadi na ndio maana tupo hapa. Tumefurahi kwa kweli, kikubwa tunaahidi kushirikiana kuendeleza shule hii,” amesema Mkurugenzi huyo.

    Akizungumza kabla ya kuanza ziara katika Shule hiyo Sylvia Lupembe, Mkuu wa Mawasiliano Serikalini Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia amesema Ujumbe huo uko nchini kuungana na watalaamu wa elimu wa hapa nchini na wa Kiswahili kwa ajili kuandaa Mpangokazi wa Utekelezaji wa Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika kuendeleza elimumsingi ikiwemo ufundishaji Kiswahili nchini Afrika Kusini.

    Hati hiyo ilisainiwa na Mawaziri wa Elimu wa nchi hizo mbili Jijini Dar es Salaam Julai 7, 2022 ambayo ilikuwa Siku ya Kiswahili Duniani.

    Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chief Albert Luthuli, Theresia Swai ameishukuru nchi ya Afrika Kusini kwa kuendeleza ushirikiano na nchi Tanzania na kuthamini mchango wa nchi yetu katika harakati za ukombozi wa nchi yao.

    Post Views: 148
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleVILIO NA MAJONZI WANAFUNZI WALIOFARIKI AJALI YA WATU 13! RAIS ATOA POLE MAGAZETI YA LEO A24TV
    Next Article MAANDAMANO YA UHAMASISHAJI WA SENSA NA MAKAZI JIJINI ARUSHA NA VIONGOZI WA DINI ,MILA

    Related Posts

    MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AMETOA MILION 33 KUNUNUA UNGA WA LISHE KWA WENYE MAHITAJI MAALUM

    February 9, 2023

    KOREA KUSINI NA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA WALETA PIKI PIKI MPYA ZA KUTUMIIA UMEME

    February 5, 2023

    BREAKING NEWS : MUSA JUMA MWENYEKITI MPYA JOWUTA SERIKALI YAAHIDI USHIRIKIANO

    January 29, 2023

    WAFANYA BIASHARA SAMUNGE JIJINI ARUSHA WAPOKEA MILLIONI 100 KUTOKA KWA NABII MKUU GEORDAVIE WAHIDI MAKUBWA KATIKA KUKUZA MITAJI YAO

    January 27, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.