Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Siasa»VIJANA WA UVCCM KATA YA LEVOLOSI WAMKATAA MWENYEKITI ALICHAGULIWA NI MAMLUKI

    VIJANA WA UVCCM KATA YA LEVOLOSI WAMKATAA MWENYEKITI ALICHAGULIWA NI MAMLUKI

    0
    By arushatv on July 25, 2022 Siasa

     

    Na Mwandishi wa A24Tv Arusha

     

     

     

     

    Vijana wa UVCCM  kata ya Levolosi jijini Arusha,wametishia kurejesha kadi za uanachama wa chama hicho na kujiunga na vyama vya upinzani baada kutoridhishwa na mwenendo wa uchaguzi uliofanyika katika ofisi ya ccm katika kata hiyo.

    Wakiongea kwa jazba mara baada ya katibu wa ccm kata hiyo,Aisha Mbaraka kutangaza matokeo,mmoja ya vijana hao,Hasan Ayub alisema kuwa hakubaliani na matokeo hayo kwani wanaami yalipangwa na mshindi aliandaliwa na hakuwa na sifa za kuchaguliwa.

    Alisema kuwa mshindi aliyetangazwa,Rasul Ramadhani aliyeshinda kwa kura 19 na kuwashinda wenzake, Hasani abdul aliyepata kura moja na Justine Renatus aliyepata kura 2,hakustahili kuwa mgombea kwa sababu hakuwa na sifa stahiki ikiwemo umri wa mgombea huyo kuwa mkubwa.

    “Kwanza wametuletea mabaunsa wakutudhibitu ,walipanga hayo matokeo hatukubali huu ni uonevu wanampitisha mtu ambaye sio mkazi wa Levolosi ”

    Naye Justine Renatus alisema kuwa hakubaliani na matokeo ya uchaguzi huo kwa kuwa anaamini yalijaa udanganyifu na mshindi alipangwa na sio mkazi wa kata hiyo na umri wake ni xaidi ya  miaka 35 kinyume na katiba inayotaka mgombea lazima awe na umri usiozidi miaka 34.

    “Sisi ndio wazaliwa wa Levolosi  huyo aliyeshinda hajulikani ni mkazi wa wapi na walimuandaa ,hatukubaliani na matokeo ya kupika tutakata rufaa na tukiona mambo ndo haya haya tunarudisha kadi”alisema Renatus

    Aliongeza kuwa amepanga kukata rufaa ngazi za juu na iwapo kama matokeo yatapaki kama yalivyo watarejesha kazi zaccm na kujiunga na vyama vingine vya upinzani.

    Hata hivyo katibu na ccm kata hiyo,Aisha Mbaraka  ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi huo aligoma kuzungumzia madai hayo hawezi kuongelea chochote kwa kuwa uchaguzi huo ni wa ndani na kwamba yeye sio msemaji wa chama.

    Aliongeza kuwa iwapo kama kuna mgombea hakulizika na matokeo hayo anaweza kukata rufaa ngazi husika.

    Katibu wa ccm wilaya ya Arusha,Kataba Sukuru aligoma kuzungumzia akisema ni uchaguzi wa ndani.

    Uchaguzi huo ni mwendelezo wa chaguzi mbalimbali zinazoendelea ndani chama cha mapinduzo huku leo umoja wa vijana uvccma wakifanya chaguzi hizo katika kata mbalimbali za jiji la Arusha.

    Post Views: 216
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleWizara ya Maliasili na Utalii imejipanga kushirikiana na Wadau  wa sekta binafsi kujadili mapendekezo ya sera,
    Next Article MSD, KUNANUKA RUSHWA WAZIRI AAGIZA KUFUMULIWA! MAGAZETI YA LEO A24TV

    Related Posts

    MRITHI WA MREMA WA TLP KUPATIKANA KESHO UCHAGUZI WAPAMBA MOTO

    March 5, 2023

    CCM NA SERIKALI SAMBAMBA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI IKUNGI

    January 17, 2023

    JUMUIYA YA WAZAZI TAIFA YAMPONGEZA RAIS SAMIA TAMKO LA MIKUTANO YA HADHARA

    January 4, 2023

    MIKUTANO YA HADHARA RUKSA IGP WAPE VIBALI MUDA WOWOTE

    January 3, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.