Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»RC MONGELA AWATAKA VIJANA KUA WAZALENDO KUWAENZI MASHUJAA

    RC MONGELA AWATAKA VIJANA KUA WAZALENDO KUWAENZI MASHUJAA

    0
    By arushatv on July 25, 2022 Habari

    Na Geofrey Stephen , Arusha

    Mavetenari waliopigana  Vita vya Kagera  (leo) wameadhimisha siku ya kumbukumbu ya mashujaa kwa kuweka silaha za jadi kwenye bustani ya Mnara wa Mashujaa Jijini Arusha.

    Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Pindi Chana sambamba Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Irrange,Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella,viongozi wa dini pamoja na wananchi.

    Akizungumza mara baada ya uwekaji wa silaha za jadi ikiwemo ngao,mkuki,shoka na sime,Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mongella alitoa rai kwa vijana kuwa wazalendo ndani ya nchi kwakuhakikisha wanalinda amani na kudumisha mashikamano.

    Ambapo Luteni Mstaafu,Allais Robert ambaye alicha nafasi yake ya uhasibu na kwenda kupigana vita vya Kagera mwaka 1978 hadi 1979,alisema wakati alipokuwa akienda vitani alikuwa na hamasa kubwa ya uzalendo wa nchi.

    Alisema alipokuwa akienda kupigana vitani alikuwa na umri wa miaka 24 na alikuwa tayari kuendana na hali halisi ya mazingira waliyokutana nayo vitani.

    “Wakati wa vita tulipata msaada kutokana kwenye vikosi mbalimbali vya majeshi yetu kutoka vyuo mbalimbali na tulijitoa kwa hali na mali kupigania nchi yetu na kumng’oa Nduli Idd Amin ”

    Alitoa rai kwa vijana kutokimbilia tamaa za fedha na maisha mazuri badala yake wafanye kazi kwa bidii na kutanguliza uzalendo mbele.

    Huku mmoja kati ya viongozi dini,Dk,Askofu ,Solomoni Masangwa wa Kanisa la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Kati (KKKT) alisisitiza amani na upendo ikiwemo kuwaombea viongozi wa serikali.

    Ends…

    Post Views: 83
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleRAIS SAMIA AWAONYA BODA BODA KUTUMIKA VIBAYA MAGAZETI YA LEO NA A24TV
    Next Article Wizara ya Maliasili na Utalii imejipanga kushirikiana na Wadau  wa sekta binafsi kujadili mapendekezo ya sera,

    Related Posts

    Kamati yapitisha makadirio ya matumizi na maendeleo 2023/2024 kwa Wizara Uwekezaji Viwanda na Biashara.

    March 23, 2023

    MWANDISHI WA HABARI MAARUFU ALLAN ISACK AITAKA NAFASI YA MNEC

    March 23, 2023

    Vyombo vya Dola na wanasheria kushirikiana kutokomeza ujangili Babati

    March 22, 2023

    JIJI LA ARUSHA LATOA MIKOPO YA SHILINGI BILION 2.6 KWA VIJANA WENYE MAITAJI MAALUM NA WANAWEKE

    March 22, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.