Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»RAIS MHE.SAMIA PAMOJA NA RAIS WA KENYA MHE.KENYATTA WAFUNGUA BARABARA YA KIKANDA YA AFRIKA MASHARIKI (ARUSHA BYPASS KM 42.4) JIJINI ARUSHA

    RAIS MHE.SAMIA PAMOJA NA RAIS WA KENYA MHE.KENYATTA WAFUNGUA BARABARA YA KIKANDA YA AFRIKA MASHARIKI (ARUSHA BYPASS KM 42.4) JIJINI ARUSHA

    0
    By arushatv on July 22, 2022 Habari

     

    Na Mwandishi wa A24Tv. Arusha 

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Arusha waliohudhuria ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) uliofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha.

       

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta, Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni, Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye, pamoja na viongozi wengine wakivuta kitambaa kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) katika Sherehe zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha.

      

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta, Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni, Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye, pamoja na viongozi wengine wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) katika Sherehe zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha 

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta wakati wa Sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha

      

    Viongozi pamoja na wananchi mbalimbali wakiwa kwenye Sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha 

     

    Kwaya ya Utumishi ikitoa burudani katika Sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha.

    .…………………………………….

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imepanga kuimarisha sekta ya bandari na sekta ya anga ili kukuza biashara ndani ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

     

    Rais Samia amesema hayo leo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass) yenye urefu wa kilomita 42.4. ambayo imegharimu shilingi Bilioni 197. 4.

     

    Aidha, Rais Samia amesema barabara hii ni muhimu kwa nchi yetu kwa kuwa ni sehemu ya barabara kuu inayounganisha kanda ya Kaskazini (Northern Corridor) hadi Holili Taveta mpakani mwa Tanzania na Kenya kuelekea Voi nchini Kenya. 

     

    Barabara hii pia inaunganisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Tanga na Kanda mbalimbali zinazounganisha Tanzania na nchi jirani za Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Zambia Sudani Kusini na Sudani hadi Ethiopia.

     

    Vile vile Rais Samia amesema kukamilika kwa barabara hii kumeimarisha sekta ya utalii pamoja na ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kijamii katika mikoa inayopita, nchi kwa ujumla, pamoja na nchi jirani. 

    Post Views: 89
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleWAREMBO MISS JUNGLE WAPONGEZA UWEKEZAJI MKUBWA WA FRANONE MINING TUTAKUA MABALOZI !
    Next Article KINA MDEE WALIA MAHAKAMANI KUITWA COVID 19 ! MAGAZETI YA LEO NA A24TV

    Related Posts

    Tanzania na India kuendeleza Uhusiano wa Kibiashara na Uwekezaji

    March 27, 2023

    TANZANIA YAKABILIWA NA UHABA WA MABAHARIA VIJANA.

    March 27, 2023

    Marcas Ajitosa kuwania U NEC Arusha

    March 25, 2023

    VIKUNDI 47 KUPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI MOITA MONDULI

    March 24, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.