Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»PURA YAIMWAGIA SIFA BODI MPYA YA TPDC, YATAKA KAZI IENDELEE

    PURA YAIMWAGIA SIFA BODI MPYA YA TPDC, YATAKA KAZI IENDELEE

    0
    By arushatv on July 5, 2022 Habari

    Na Ahmed Mahmoud

    Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa mkondo wa juu wa Petroli (PURA),Mhandisi Charles Sangweni amesema kuwa kupatikana kwa bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli hapa nchini(TPDC) kutasaidia mamlaka yao kuongeza majukumu ,udhibiti na wigo mpana katika usimamizi wa sekta hiyo.

    Pia amesema kwamba anaamini kupatikana kwa bodi ya TPDC kutasaidia kuongeza idadi ya mikataba na makampuni ya Utafiti wa mafuta nchini ambako kwa Sasa Kuna Jumla ya mikataba 11 na makampuni 8.

    Mhandisi Sangweni alitoa kauli hiyo Wakati akihojiwa na waandishi wa habàri mara baada ya Waziri wa nishati nchini, January Makamba kuzindua bodi ya TPDC Jijini Arusha.

    Akiongea na waandishi wa habàri Mhandisi Sangweni alisema kuwa PURA kama wathibiti wanaamini ya kwamba kupatikana kwa bodi ya TPDC kutasaidia kuongeza majukumu katika eneo la usimamizi wa mafuta.

    “Tuna mikataba 11 na makampuni 8 kama TPDC itakwenda kwa kasi tunaamini idadi ya makampuni itaongezeka sisi kama wathibiti hii itatuongezea majukumu” alisema Mhandisi Sangweni

    Hatahivyo, alisema kwamba kupitia sheria ya Petroli ya Mwaka 2015 kipengere Cha 50 imempa mamlaka Waziri wa nishati kuipendelea TPDC na kuikabidhi vitalu vya mafuta kuviendesha bila kufungua zabuni hivyo anaamini kupitia sheria hiyo Shirika hilo litatumia fursa hiyo kuongeza vitalu kadhaa.

    Naye Mkurugenzi Mkuu wa TPDC , James Mataragio alisema kuwa Shirika lao liko katika Mchakato wa Utafiti wa uchimbaji wa mafuta katika eneo la Eyasi -Sombele mkoani Manyara na tayari wameshachimba visima vifupi vitatu ambapo wamekusanya taarifa ya usumaku wa ramani ya kijographia kupitia ndege Mwaka 2015.

    Mataragio, alisema kuwa taarifa katika eneo hilo zinaonyesha kuwa Kuna uwezekano mkubwa wa eneo hilo kuwa na mafuta na tayari TPDC wameshatangaza zabuni ya kuchukua taarifa za mitetemo ili kupata eneo la kuchimba mafuta.

    Huu ni Mradi wenye matumaini sana baada ya miaka miwili tutakuwa kwenye nafasi nzuri ya ugunduzi wa mafuta kama majirani wenzetu Kenya na Uganda waliopata mafuta katika eneo la bonde la ufa” alisema Mataragio

    Post Views: 64
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleSIASA BANDARINI ! MKURUGENZI ATUMBULIWA MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV
    Next Article SHULE ZA SERIKALI KIDEDEA MATOKEO KIDATO CHA 6 MAGAZETI YA LEO NA A24TV

    Related Posts

    Kamati yapitisha makadirio ya matumizi na maendeleo 2023/2024 kwa Wizara Uwekezaji Viwanda na Biashara.

    March 23, 2023

    MWANDISHI WA HABARI MAARUFU ALLAN ISACK AITAKA NAFASI YA MNEC

    March 23, 2023

    Vyombo vya Dola na wanasheria kushirikiana kutokomeza ujangili Babati

    March 22, 2023

    JIJI LA ARUSHA LATOA MIKOPO YA SHILINGI BILION 2.6 KWA VIJANA WENYE MAITAJI MAALUM NA WANAWEKE

    March 22, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.