Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Business»Prof: Kahyarara: Biashara kati ya Tanzania na Kenya Yaongezeka

    Prof: Kahyarara: Biashara kati ya Tanzania na Kenya Yaongezeka

    0
    By arushatv on July 7, 2022 Business

    Na Mwandishi wa A24Tv .

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara amesema biashara kati ya Tanzania na Kenya imekuwa zaidi baada ya ya makubaliano kati ya Tanzania na Kenya kuondoa vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru 49 kati ya 64 wakati vikwazo vingine 15 vilivyobaki vinafanyiwa kazi.

    Prof. Kahyarara ameyasema hayo Julai 6, 2022 wakati wa kipindi cha Morning Trumpet kinachoendeshwa na Kituo cha Televisheni cha Azam, jijini Dar es salaam

    Amesema katika kipindi cha mwaka mmoja (1) na miezi mitatu (3) cha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, uwekezaji umeongezeka kutoka bilioni 1 hadi bilioni 9 na Kituo cha uwekezaji kimesajili wawekezaji 380 wa ndani na nje ya nchi.

    Aidha, Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kutekeleza Mpango wa kuboresha mazingira ya biashara kwa kufuta tozo na kufanya marekebisho ya sera na sheria mbalimbali ili kuvutia wawekezaji na wafanyabiasha nchini na kuongeza ajira, pato la taifa na kukuza uchumi kwa ujumla. Amesema Prof. Kahyarara.

    Akitolea mfano wa kongani ya viwanda ya Kwala iliyopo Kibaha inayotarajiwa kutoa ajira 100,000 za moja kwa moja na 500,000 zisizo za moja kwa moja, Prof. Kahyarara amesema Serikali inalenga kuwa na viwanda vikubwa vingi vitakavyoanzishwa katika kongani za viwanda mbalimbali nchini kwa lengo la kuongeza ajira, pato la taifa na mauzo ya nje.

    Aidha, amesema Serikali imeanzisha Mfumo wa Kielektroniki wa Huduma za pamoja kwa Wawekezaji unaounganisha taasisi 12 zinazohusika kuhudumia wawekezaji ili kupunguza urasimu na changamoto mbalimbali katika uwekezaji na kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo.

    Pamoja na Mfumo huo, Serikali pia imeanzisha Mfumo unaroa huduma za uhamiaji kwa mtandao hususan utoaji wa vibali vya Ukaazi (e-Permit) na Vibali vya kufanya kazi nchini kwa kuzingatia soko la ajira.

    Katika kutatua changamoto ya uhhaba wa mafuta ya kula, Prof Kahyarara pia amesema Serikali inachukua hatua mbalimbali za kuongeza uzalishaji wa mazao yanayotoa mafuta ya kula pamoja na kuwawezesha wananchi kumiliki viwanda vidogo na vya kati vya kuchakata mafuta hayo kupitia Programu maalumu ya Total Industrial Solution inayowawezesha wananchi kumili kiwanda ndani ya muda mfupi kwa gharama nafuu

    Post Views: 60
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleWAZIRI MKUU WANANCHI WAISHI KWA AMANI ! MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV
    Next Article KAMATI YA YA BUNGE YA BAJETI YAMPONGEZA RAIS KWA FEDHA ZA USTAWI WA TAIFA

    Related Posts

    WAZIRI MKENDA AZINDUA MKOPO WA ELIMU KUTOKA BENK YA NMB.

    March 15, 2023

    Tanzania na China Kuendeleza Uhusiano wa Kibiashara

    February 27, 2023

    RC MAKALA AISHUKURU BENKI YA NMB KUZAMINIA ZIARA YA VIONGOZI MACHINGA NA BODABODA RWANDA.

    February 4, 2023

    BANK YA UBA YAFIKA ARUSHA WAFANYA BIASHARA WAFURAIYA RIBA NAFUU

    January 20, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.