Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»NEEMA YAJA KWA UPANDE WA VIATILIFU NA AFYA

    NEEMA YAJA KWA UPANDE WA VIATILIFU NA AFYA

    0
    By arushatv on July 2, 2022 Habari

    Na mwandishi wa A24Tv .

    Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe Dkt.Ashatu Kijaji (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Mhe. Bruno Rodriguez Parrilla kuhusu uwezekano wa kupanua zaidi kiwanda cha kuzalisha viwatilifu ili kuzalisha bidhaa ya mbolea pamoja na bidhaa zingine za Afya.

    Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Waziri Kijaji amesema moja ya bidhaa ambayo wanataka kuzalisha kwennye kiwanda cha Labiofam kilichopo Kibaha mkoani Pwani ni mbolea ambayo itakayowezesha kuwa na utoshelevu wa mbolea ndani ya Taifa letu.

    “Kilimo ni sekta ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa kwenye uchumi wa Taifa letu hivyo mbolea ni moja ya ya malighafi muhimu kuhakikisha kilimo kinakuwa na mchango mkubwa kwenye uchhumi wa Taifa letu, sisi kama Wizara tuko tayari kuhakikisha kiwanda chetu kinaendelea na uuzalishaji wa bidhaa hizi muhimu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu”. Amesema Waziri Kijaji.

    Aidha, Waziri Kijaji amesema majadiliano kati ya Serikali ya Tanzania na Cuba yanatarajiwa kuanza hivi karibuni na timu za wataalamu kwa nchi zote mbili zimeundwa na zipo tayari kuanza majadiliano mara baada ya wataalamu kutoka cuba kuingia nchini kuanzia Julai 8 hadi 10.

    Naye, Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Mhe. Valentino Mlowola amesema manufaa ya ugeni kutoka nchini Cuba utasaidia kupanua ushirikiano kati ya nchi hizo hasa katika sekta ya afya, elimu, viwanda na kilimo ambazo zitaongeza ajira kutokana na uwekezaji utakaofanywa baina ya nchi hizo.

    “Uhusiano wetu na Cuba ni mzuri na unaendelea kuimarika siku hadi siku na tutaendelea kushirikiana kwenye sekta mbalimbali hususani kwenye sekta yya afya,Elimu pamoja na Viwanda”. Amesema Balozi Mlowola

    Post Views: 72
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleBINTI WA KITANZANIA RAWAN DAKIKI AWEKA HISTORIA NYINGINE KUPANDA MLIMA MKUBWA DUNIANI
    Next Article WAZIRI KIJAJI USO KWA USO NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE CUBA,

    Related Posts

    Tanzania na India kuendeleza Uhusiano wa Kibiashara na Uwekezaji

    March 27, 2023

    TANZANIA YAKABILIWA NA UHABA WA MABAHARIA VIJANA.

    March 27, 2023

    Marcas Ajitosa kuwania U NEC Arusha

    March 25, 2023

    VIKUNDI 47 KUPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI MOITA MONDULI

    March 24, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.