Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Break News»NCHI ZINAZOZALISHA ALMASI BARANI AFRIKA(ADPA )ZAKUBALIANA KUFANYA MAREKEBISHO YA KATIBA YA UMOJA HUO.

    NCHI ZINAZOZALISHA ALMASI BARANI AFRIKA(ADPA )ZAKUBALIANA KUFANYA MAREKEBISHO YA KATIBA YA UMOJA HUO.

    0
    By arushatv on July 29, 2022 Break News

     

    Na .Mwandishi wanA24Tv Arusha

    Umoja wa nchi zinazozalisha almasi barani Afrika (ADPA) zimekubaliana kupitia upya na kurekebisha katiba na miongozo ya umoja huo kwa kuwa ile ya awali inepitwa na wakati.

    Hayo yamesemwa leo na waziri wa madini nchini,Dotto Biteko katika mkutano wa ADPA unaondelea jijini Arusha.

    Akizungumza na waandishi wa habari Waziri Biteko alisema kwamba tayari timu ya wataalamu imeshakamilisha nyaraka ambapo wataziwasilisha kwenye baraza la mawaziri ili ziweze kupitiwa .

    Waziri Biteko alisema kwamba wamejiridhisha kwamba nyaraka hizo zinahitaji marekebisho ili ziweze kuendana na wakati.

    “Leo zege halilali tunataka kuhakikisha tunakamilisha nyaraka za kuongoza ADPA ili kupitisha katiba iendane na wakati “alisema Biteko

    Waziri Biteko alisisitiza kwamba umoja huo leo unataraji kukamilisha kazi ya kuajiri watendaji kwa kuwa waliokuwepo wametoa nchini Angola na wanafanya kazi kama hisani.

    “Kazi tuliyonayo leo pia tuna agenda ya kuajiri watendaji kwani waliokuwepo wanatokea Angola na wanafanya kazi kama hisani hatuwezi kuwa na umoja wenye nguvu wakati una watendaji wa kuazima “alisisitiza Waziri Biteko

    Hatahivyo,waziri Biteko alisisitiza kwamba mbali na umoja huo kuwa na wanachama 19 tayari kuna nchi 6 barani Afrika zimeomba kujiunga na mchakato bado unaendelea.

    Mwisho.

    Post Views: 56
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleUGONJWA WA SARATANI BADO TISHIO NCHINI TAKWIMU ZAONGEZEKA
    Next Article MSHAHARA MPYA SERIKALI YATOA TAMKO ! MAGAZETI YA LEO NA A24TV

    Related Posts

    MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AMETOA MILION 33 KUNUNUA UNGA WA LISHE KWA WENYE MAHITAJI MAALUM

    February 9, 2023

    KOREA KUSINI NA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA WALETA PIKI PIKI MPYA ZA KUTUMIIA UMEME

    February 5, 2023

    BREAKING NEWS : MUSA JUMA MWENYEKITI MPYA JOWUTA SERIKALI YAAHIDI USHIRIKIANO

    January 29, 2023

    WAFANYA BIASHARA SAMUNGE JIJINI ARUSHA WAPOKEA MILLIONI 100 KUTOKA KWA NABII MKUU GEORDAVIE WAHIDI MAKUBWA KATIKA KUKUZA MITAJI YAO

    January 27, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.