Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»Chama cha walimu Mkoa wa Arusha(CWT)Imeiyomba serikali kuboresha Maslai ya walimu

    Chama cha walimu Mkoa wa Arusha(CWT)Imeiyomba serikali kuboresha Maslai ya walimu

    0
    By arushatv on July 18, 2022 Habari

    Na Geofrey Stephen .ARUSHA

    Chama cha walimu Mkoa wa Arusha(CWT)kimeitaka serikali kuhakikisha  inaboresha maslahi bora ya walimu ikiwemo mazingira mazuri ya kufundishia na kulipa stahiki za walimu kwa wakati pindi wanapohamishwa vituo vya kazi.

    Akiongea na waandishi  wa habari katika kikao kazi cha wafanya maamuzi ngazi ya halmashauri na Mkoa,mwenyekiti  wa CWT mkoani hapa,Mwl.Lotta Laizer alisema kuwa pamoja na Rais Samia Sululu  Hasani kujitahidi kutatua baadhi ya changamoto ikiwemo nyongeza ya mshahara lakini bado hangamoto  ni kubwa.

    Laizer  alisema kuwa serikali kama mwajiri wa walimu nchini inawajibu wa kuhakikisha walimu wanapata stahiki zao sahihi kwa wakati jambo litakalo saidia kuongeza morari wa kufundisha na kuongeza ufaulu nchini.

    “Kuna changamota  nyingi ambazo kimsingi  mwalimu anastahili kuzipata ikiwemo,mfumo wa taarifa ,mabadiliko ya zama,kucheleweshwa kwa stahiki za walimu ,sheria kandamizi za kazi “alisema .

    Hata hivyo alimpongeza Rais Samia  kwa kuwaongezea mishahara  walimu na kupunguza baadhi ya changamoto zilizokuwa zikiwakabili kwa muda mrefu.

    Katibu wa CWT,Abraham  Kamwela,alisema kikao hicho kiliwashirikisha viongozi wa CWT Mkoa na wilaya ,wafanya maamuzi wakiwemo wakurugenzi wa halmashauri wakuu wa wilaya na makatibu wakuu wa wilaya ,maafisa elimu na utumishi lengo likiwa ni kufahamishana mabadiliko mbalimbali ya sheria.

    “Kwa mfano sheria ya ajira na Mahusiano kazini inayo mabadiliko kadhaa inayohusiana na uendeshaji wa vyama vya wafanyakazi,hivyo tukikaa pamoja tunaweza kutafisiri mabadiliko hayo na kuondoka na Jambo moja”alisema.

    Naye kaimu afisa elimu Mkoa wa Arusha,Shelley Swai alisema mkoa wa Arusha unachangamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa walimu wa shule za msingi na serikali.

    Alisema mkoa wa Arusha unauhitaji wa walimu 8573 na waliopo ni 6738 tu,hivyo upungufu ni walimu 1793 .

    Awali kaimu katibu tawala mkoa wa Arusha David  Lyamongi alisema mkoa wa Arusha umekuwa ukifanya vizuri kwa matokeo mazuri ya ufaulu kutokana na jitihada zinazofanywa na wadau wa elimu.

    Lyamongi aliwasisitiza CWT kuweka mazingira mazuri na mahusiano baina ya serikali na chama Cha walimu ili  kuondoa mivutano kati ya mwajiri na chama hicho hasa kuhusu suala la masilahi.

    Ends…

    Post Views: 433
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleLIPUMBA AMWAGIA SIFA RAIS SAMIA KWA UTAWALA BORA MAGAZETI YA LEO A24TV
    Next Article RC Mongela Aionya Halmashauri ya Arusha DC Aitaka kuongeza Mapato

    Related Posts

    Kamati yapitisha makadirio ya matumizi na maendeleo 2023/2024 kwa Wizara Uwekezaji Viwanda na Biashara.

    March 23, 2023

    MWANDISHI WA HABARI MAARUFU ALLAN ISACK AITAKA NAFASI YA MNEC

    March 23, 2023

    Vyombo vya Dola na wanasheria kushirikiana kutokomeza ujangili Babati

    March 22, 2023

    JIJI LA ARUSHA LATOA MIKOPO YA SHILINGI BILION 2.6 KWA VIJANA WENYE MAITAJI MAALUM NA WANAWEKE

    March 22, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.