Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Uncategorized»WFP yawatajirisha wananchi wa Kigoma .yanunua mazao Yao,watoa elimu kilimo Bora,yajenga maghala.

    WFP yawatajirisha wananchi wa Kigoma .yanunua mazao Yao,watoa elimu kilimo Bora,yajenga maghala.

    0
    By arushatv on June 13, 2022 Uncategorized

    Mwananchi wetu.

    Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), kupitia Mradi wa Kigoma Pamoja (KJP), limefanikiwa Kuwatajirisha wananchi mkoani Kigoma kwa kununua mazao yao wanayozalisha,kuwajengea maghala na kuwapatia mashine za kuwasaidia kuandaa mazao.
    Miradi hiyo inatekekezwa Kwa kushirikisha mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) mbali ya WFP, ni pamoja na Kituo cha Biashara cha Kimataifa (ITC), Shirika la Uendelezaji wa Mitaji la Umoja wa Mataifa (UNCDF) na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO).
    Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Rashidi Mchatta alisema WFP ni moja ya mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) yamekuwa na Manufaa makubwa kwa wananchi kwa Kigoma .

    Mchatta Pia alisema WFP wameanzasha vyama vya ushirika na kuviunganisha na masoko, hivyo wakulima Wana uhakika na soko

    ” WFP wametoa elimu na kuwawezesha maofisa ugani kuwa karibu na wakulima, hivyo wamechangia ongezeko la mazao”alisema

    Mchatta alisema Serikali ya mkoa itahakikisha mafanikio hayo yanaendelezwa na kusambazwa kwa wakulima wote mkoani hapO.

    Mratibu wa KJP Wilaya ya Kasulu, Masalu Charahani wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii ambaye alikuwa katika ziara ya kuangalia namna mradi huo ulichangia mafanikio kwa wakulima na halmashauri.

    Charahani amesema kabla ya mradi huo kufika Halmashauri ya Mji Kasulu kilimo cha maharagwe na mahindi kilikuwa kinachangia mapato kidogo ila kwa miaka miwili ya mradi mapato yameongezeka kwa kiwango kikubwa.

    “Kabla ya mradi ushuru wa zao la maharagwe ulikuwa hauzidi Sh.milioni 150 ila kupita elimu na mafunzo waliyopata wakulima tunakusanya ushuru hadi Sh.milioni 200. Hivyo hivyo kwenye mahindi tulikuwa tunakusanya Sh.milioni 50 ila sasa tunakusanya zaidi ya Sh.milioni 100,” alisema.

    Amesema WFP, FAO, UNCDF na ITC wamehusika kwa asilimia kubwa kwa Halmashauri Mji Kasulu kuongeza mapato, hivyo watahakikisha hawayaangushi mashirika hayo ya kimataifa.

    Charahani ameongeza kuwa WFP imekuwa ikitoa elimu kuhusu namna ya kuvuna, kuhifadhi na kuwapatia wakulima vifaa kama maturubai, mashine ya kupima unyevu, mashine za kupukuchua mahindi na mengine mengi.

    Amesema WFP kwa kushirikiana na Serikali wametoa mafunzo ya namna ya kuandaa shamba, kuvuna na kuhifadhi mazao kwa wakulima 3,000.

    Alisemawamepokea mashine tatu ya kupukuchua mahindi,kutoka WFP ambapo mashine hizo zinaweza kupukuchua magunia 25 kwa saa mbili na kutumia lita moj ya mafuta ya diZeli hivyo ukiwa na lita mbili unapukuchukua gunia 50 za mahindi.

    Akizungumza kuhusu mradi huo Mzee Sospeter Mkula wa Kijiji cha Nyumbigwa alisema WFP wamemuwezesha kulima kilimo cha kisasa ambapo anatumia eneo dogo anapata mavuno mengi.

    “Nawashukuru WFP na wadau wengine ambao wametujengea uwezo wa namna ya kuandaa shamba, kuvunia, na kuhifadhi. Elimu hii imesadia kupata mazao bora ambayo thamani yake inakuwa juu,” alisema.

    Kwa upande wake Mirambo Masudi alisema mradi huo wa KJP ambao unatekelezwa na WFP umemuongezea hamasa ya kutaka kulima kwani ana uhakika wa kupata chakula cha familia yake na soko ndani na nje ya nchi.

    “Sisi tulikuwa tukivuna tunayatupa chini, matokeo yake mahindi yanakuwa machafu na hayana ubora unaohitajika, hivyo tunakula chakula kichafu, lakini baya zaidi hata kama unataka kuuza unauza kwa bei ndogo,” alisema.

    Mkuu wa Programu za WFP wilayani Kasulu, Michael Bisama alisema uwekezaji waliwekeza umetoa matokeo chanya hivyo kuiomba Serikali kuendeleza mpango huo

    Bisama Alisema wananchi tayari wameanza kunufaika na Kilimo Chao lakini pia maisha Yao yamebadilika sana kutokana na utekelezaji wa mradi huu wa Kigoma Pamoja.

    Mwisho

    Post Views: 100
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleCORRDO SPRING HOTEL YAMALIZA DENI LA BILIONI 13 SASA HIKO MIKONO SALAMA !
    Next Article KESI YA KINA MDEE YAANZA KUNGURUMA MAHAKAMANI NI MVUTANO MKALI ! MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV

    Related Posts

    SHEHENA LA MBOLEA ILIYO JAZWA MCHANGA YAKAMATWA WAZIRI ATOA MAAGIZO MAZITO

    March 5, 2023

    Wadau wa Tehama mkoani Arusha watakiwa kutoa ushirikiano kuhakikisha uwepo wa kituo cha ubunifu wa Tehama.

    February 28, 2023

    KATIBU TAWALA MKOA WA ARUSHA ASISITIZA MAFUNZO KUTOKA TUME YA USHINDANI NCHINI

    February 23, 2023

    TANESCO NCHINI KUTEKELEZA MIRADI YA UZALISHAJI UMEME, KUONDOA CHANGAMOTO KWA JAMII

    February 23, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.