Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Break News»Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano Biashara na Uwekezaji wa bunge la jumiya ya Afrika Mashariki EALA , amezitaka nchi za Jumuiya kuzisisitiza Idara za uhamiaji za nchi zao kufuata sheria ya utoaji wa viza.

    Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano Biashara na Uwekezaji wa bunge la jumiya ya Afrika Mashariki EALA , amezitaka nchi za Jumuiya kuzisisitiza Idara za uhamiaji za nchi zao kufuata sheria ya utoaji wa viza.

    0
    By arushatv on June 9, 2022 Break News

    Na GeofreyvStephen ARUSHA

    Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano Biashara na Uwekezaji wa bunge la jumiya ya Afrika Mashariki EALA , Christopher Nduwayo amezitaka nchi za Jumuiya hiyo kuzisisitiza Idara za uhamiaji za nchi zao kufuata sheria ya Jumuiya hiyo inayoelekeza suala la utoaji wa viza.

    Akiwasilisha Taarifa ya kamati hiyo mbele ya Bunge hilo linaloendelea makao makuu ya EAC jijini Arusha,alisema kuwa ipo haja kubwa ya kuangalia suala zima la utoaji wa viza hususani kwa wananchi wanachama ambalo lonaonekanankuwa bado linachangamoto kwa wananchi pindi wanaposafiri katika nchi hizo .

    Alisema kumekuwepo na changamoto ya Maafisa uhamiaji katika maeneo ya mipaka kuendelea kutoa viza ya siku Saba wengine mwezi ambapo ni kinyume na utaratibu wa sheria iliyopitishwa na nchi hizo.

    “Unakuta Mwananchi anatoka Burundi anapewa viza ya siku Saba na Mwananchi huyo mfano anaenda nchi Tanzania Jijini Dar es Salaam kufika huko lazima atumie siku mbili za kwenda hapo anabakiza siku tano kufanya biashara kwa siku hizo hadi kurudi mpakani ni siku chache inayopelekea akifaka mpakani kulipa faini hii ni usumbufu kwa Mwananchi”alisema

    Alibainisha kwamba ni vyema kila nchi ikafuata utaratibu wa sheria ulipitishwa na nchi hizo za Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kuwapa viza ya miezi sita kila mwananchi anayetaka kusafiri ili kupunguza usumbufu unaoendelea kujitokeza katika mipaka na kuwatia hofu ya kufanyabiashra.

    “Jumuiya yetu imeundwa kwa ajili ya kuwasaidia na kuondoa vikwazo vya kibiashara kwa Wafanyabishara wanaozunguka katika kufanya biashara zao eneo Moja la nchi Moja hadi nyingine kupitia mipaka ya nchi za Jumuiya” Alisema Nduwayo.

    Alisema kwa ipo haja ya kuangalia pia suala zima la vibali vya kazi ambapo wafanyakazi wa kazi ndogondogo Jumuiya iliafiki waruhusiwe kufanyakazi lakini bado wamekuwa wakipata vikwazo mbalimbali wanapovuka mipaka ya nchi zetu.

    “Mfano Mimi ni mbunge nilipita katika Moja ya mpaka wakanigongea kibali cha mwezi Moja tena baada ya kuuliza kihusiana na sheria hiyo ya miezi sita na bado katika Passipoti yangu waliniandikia kitofanyakazi popote Sasa nashangaa Mimi ni Mbunge na huku nakuja kufanyakazi ya kuwatumikia wananchi wa Jumuiya ni vyema serikali zetu zikaa na kutoa Elimu ya kutosha kwa maafisa Hawa wa Uhamiaji hususani katika mipaka yetu”alisema

    Kwa Upande wake Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Dkt. Abdullah Makame alisema kwamba baadhi ya mipaka katika vituo vya mipakani hakuna makazi ya watumishi wakiwemo Uhamiaji TRA na Polisi ambapo inapelekea wafanyakazi wa Idara hizo kufanyashighuli zao bila ufanisi.

    Alisema Kutokana na hilo ni vyema kila nchi itengeneze utaratibu wa kuwajengea nyumba au makazi yenye viwango watumishi wao kwenye vituo hivyo ili wafanyekazi kwa ubora na ufanisi mkubwa.

    ” Aidha katika kipaumbele alichopanga Katibu Mkuu  wa Jumuiya hiyo alipoingia katika nafasi yake alipanga kazi yà kwanza ni kuongeza mwanachama mpya Jambo ambalo amelitekeleza kwa kumpata DRC CONGO ambayo inamalizia utaratibu ili kuingia rasmi baada ya hilo kazi nyingine kubwa aliopanga ni kuunda kamati ya biashara ya Afrika Mashariki ili kuokoa watu wa sekta binafsi”alisema.

    Aliongeza kuwa atatumia nguvu kuhakikisha kwa Mwaka huu kamati hiyo inapatikana ili kupunguza tatizo la Kodi mipakani pamoja na changamoto zake.

    Ends…

    Post Views: 44
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleSERIKALI YAKIHAKISHIA KIWANDA CHA KAGERA SUGAR MAZINGIRA YA UWEZESHAJI WA UZALISHAJI WA SUKARI
    Next Article WABUNGE WA EALA WATOA MAONI YAO KUPUNGUA KWA BAJETI YA EAC MJADALA MZITO BUNGENI

    Related Posts

    MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AMETOA MILION 33 KUNUNUA UNGA WA LISHE KWA WENYE MAHITAJI MAALUM

    February 9, 2023

    KOREA KUSINI NA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA WALETA PIKI PIKI MPYA ZA KUTUMIIA UMEME

    February 5, 2023

    BREAKING NEWS : MUSA JUMA MWENYEKITI MPYA JOWUTA SERIKALI YAAHIDI USHIRIKIANO

    January 29, 2023

    WAFANYA BIASHARA SAMUNGE JIJINI ARUSHA WAPOKEA MILLIONI 100 KUTOKA KWA NABII MKUU GEORDAVIE WAHIDI MAKUBWA KATIKA KUKUZA MITAJI YAO

    January 27, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.