Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Break News»Mbunge alia na barabara ya mchepuko kukwepa maporomoko ya Sonni

    Mbunge alia na barabara ya mchepuko kukwepa maporomoko ya Sonni

    0
    By arushatv on June 5, 2022 Break News

    Na Joseph Ngilisho, Lushoto.

    Mbunge wa Jimbo la Lushoto,mkoani Tanga,Shaaban Shekilindi ameishauri serikali kukamilisha ujenzi wa barabara ya mchepuko kwa kiwango cha Lami ili kuondoa changamoto ya Mara kwa Mara inayotokana na maporomoko ya mawe kwa barabara kuu inayotoka Mombo Hadi Lushoto ambayo imekuwa kilio kikubwa kwa wafanyabiashara wa mazao na mbogamboga pindi inapoziba.

    Aidha ameishauri serikali kuangalia namna ya kuwachukukia hatua Kali makandarasi wanaochelewesha miradi mbalimbali ya maendeleo na kusababisha wananchi kuendelea kuteseka kwa kukosa huduma ya usafiri Katika wilaya hiyo.

    Shekilindi ametoa kilio hicho mwishoni mwa wiki mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa,Sahili Geraruma wakati Mwenge wa Uhuru ulipofika jimboni kwake kutembelea,kuzindua na kuweka jiwe la msingi Katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
    Alisema kwa muda mrefu amekuwa akilalamikia serikali na Bungeni mradi wa barabara ya mchepuko yenye urefu wa kilometa 16 inayoanzia Dochi kupitia  Nguli hadi Mombo ili kuwarahisishia wananchi na wafanyabiashara wanaosafirisha mazao kupita kwa urahisi tofauti na ilivyo sasa.
    Alisema kuwa wananchi wa maeneo hayo wanategemea barabara moja pekee inayotoka Mombo kupitia Sonni hadi Lushoto barabara ambayo kunapotokea maporomoko barabara hiyo huziba na kutopitika na hivyo kuwa changamoto kubwa kwa wananchi na Wafanyabiashara.
    Akiongelea suala la wakandarasi wanaotekeleza miradi  Katika Jimbo lake ,alisema wamekuwa changamoto ya ucheleweshaji wa miradi ya barabara kutokana na visingizio kadhaa visivyo na tija hivyo amewataka wakandarasi hao kumaliza kazi kwa wakati Kama mkataba unavyoeleza na kusema changamoto zilizo Nje ya Mkataba hazitakubalika kwani ni kuwaweka wananchi Katika hali mbaya kiusafiri.
    Naye mkandarasi wa kampuni ya ujenzi ya  KIV  (KIV Company LTD) , Joseph Malumbo ,anayetekeleza mradi wa barabara yenye urefu wa kilometa moja  kwa kiwango Cha lami,alimshukuru kiongozi wa mbio za mwenge ,kuutembelea mradi huo na kuridhishwa na hatua iliyofikiwa.
    Malumbo aliongeza kuwa mradi huo unagharimu kiasi Cha Shilingi milioni 493,271,000 alitarajia kukamilisha juni 19 Mwaka huu lakini kutokana na changamoto ya mvua  na kuhamisha udongo unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi huu.
    Naye kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa, Sahili Geraruma aliwataka wakandarasi hao kuhakikisha wanakamilisha miradi ya serikali kwa wakati na kwa kuzingatia ubora unaohitajika na wawe wazalendo kwa sababu wao ni  wazawa.
    Mkuu wa wilaya ya Lushoto,Kalisti Lazaro alisema kuwa atahakikisha anayafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na kiongozi wa mbio za mwenge 2022, ikiwemo matumizi sahihi ya fedha zinazotolewa na serikali na ubora wa mradi.
    Post Views: 121
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleRAIS SAMIA AWAPA NEEMA MAKANDARASI WA NDANI MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV
    Next Article MBOWE AELEZA SABABU ZA KUKOMALIA KATIBA MPYA MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA

    Related Posts

    MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AMETOA MILION 33 KUNUNUA UNGA WA LISHE KWA WENYE MAHITAJI MAALUM

    February 9, 2023

    KOREA KUSINI NA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA WALETA PIKI PIKI MPYA ZA KUTUMIIA UMEME

    February 5, 2023

    BREAKING NEWS : MUSA JUMA MWENYEKITI MPYA JOWUTA SERIKALI YAAHIDI USHIRIKIANO

    January 29, 2023

    WAFANYA BIASHARA SAMUNGE JIJINI ARUSHA WAPOKEA MILLIONI 100 KUTOKA KWA NABII MKUU GEORDAVIE WAHIDI MAKUBWA KATIKA KUKUZA MITAJI YAO

    January 27, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.