Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»CAMARTEC MBIONI KUANZISHA KITOVU CHA ZANA ZA KIHANDISI MKOA WA SIMIYU.

    CAMARTEC MBIONI KUANZISHA KITOVU CHA ZANA ZA KIHANDISI MKOA WA SIMIYU.

    0
    By arushatv on June 6, 2022 Habari

    Na Mwandishi wa A24Tv

    Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara upande wa Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amesema Kitovu cha teknolojia za zana za kilimo kitakachoanzishwa Wilaya ya Maswa kitaongeza tija ya uzalishaji wa mazao mbalimbali ya kilimo kuanzia maandalizi ya shamba, uvunaji na uchakataji wa mazao hayo.

    Dkt Hashil ameyasema hayo Juni 4, 2022 alipotembelea Jengo  la raslimali za kilimo lililopo kijiji cha Mwandete Wilaya ya Maswa litakalotolewa kwa  Kituo cha Zana za Kilimo na Ufundi Vijijini  (CAMARTEC) kwa ajili ya kuanzisha Kitovu cha teknolojia za Kihandisi kitakachotoa huduma za mafunzo na zana za kilimo wilayani humo.

    [6/5, 11:40 PM] Pro Wizara Ya Biashara: Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara upande wa Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiongea na Wananchi wa Kijiji cha Mwandete  Wilaya Maswa ujio wa kitovu cha zana za kilimo kitakachoongeza tija katika mazao yao kwa kutumia zana zenye teknolojoa rahisi Juni 4 2022.
    [6/5, 11:42 PM] Pro Wizara Ya Biashara: Mkurugenzi  Mtendaji wa  Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Bw . Simon Berege  akiongea na Wananchi wa Kijiji cha Mwandete  Wilaya Maswa ujio wa kitovu cha zana za kilimo kitakachoongeza tija katika mazao yao kwa kutumia zana zenye teknolojoa rahisi Juni 4 2022.Dkt. Hashil akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda, Dkt. Wilson Lugano, Kaimu Mkurugenzi wa CAMARTEC  pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa walipata fursa ya kuongea na wanakijiji cha Mwandete  waliofurahishwa na ujio wa kitovu hicho cha zana za kilimo kitakachoongeza tija katika mazao yao kwa kutumia zana zenye teknolojoa rahisi.
    Naye Mkurugenzi  Mtendaji wa  Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Bw . Simon Berege  amesema  Halmashauri hiyo iko katika makubaliano na CAMARTEC   kuanzisha kitovu hicho cha teknolojia za kihandisi ambacho kitaongeza tija katika mazao ya kilimo hasa mazao yanayotoa malighafi viwandani ikiwemo  Pamba na alizeti katika wilaya hiyo na mkoa wa Simiyu kwa ujumla.

    Aidha, Mkurugenzi huyo amesema halmashauri yake iko tayali kuwawezesha wakulima kupata zana hizo kwa mikopo yenye riba nafuu kupitia mifuko mbalimbali ili waweze kupata zana hizo na kuzitumia  katika shughili zao za kilimo na hatimaye kuongeza tija katika nazao yao, ajira na kipato.

    Aidha  akitoa taarifa fupi ya maendeleo ya sekta ya Viwanda na biashara kwa Naibu Katibu Mkuu, Mkurugenzi huyo amesema Wilaya hadi sasa ina  viwanda vikubwa 5, vya kati 3 na vidogo vidogo 204. Kati ya Viwanda hivyo Halimashauri inamiliki Kiwanda cha kusindika unga wa viazi lishe, Kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi  na Kiwanda cha kukoboa mpunga na kupanga madaraja ya mchele.

    Kaimu Mkurugenzi wa CAMARTEC Mhandisi Pythias Ntella akiongea na Wananchi wa Kijiji cha Mwandete  Wilaya Maswa ujio wa kitovu cha zana za kilimo kitakachoongeza tija katika mazao yao kwa kutumia zana zenye teknolojoa rahisi Juni 4 2022.

    Awali Kaimu Mkurugenzi wa CAMARTEC Mhandisi Pythias Ntella Lengo la kuanzisha kituo hicho ni kutoa mafunzo na kuunda mashine ambazo zinahitajika katika maeneo hayo hasa zana za maandalizi ya shamba kama trekta,  mashine za kupura alizeti na mtama, mashine za  kukata na kufunga malisho ya mifugo,  mashine za vipandio na  nyingine nyingi  kulingana na mahitaji halisi ya wakulima na wafugaji mkoani humo na mikoa yote kwa ujumla.

    Post Views: 143
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleMBOWE AELEZA SABABU ZA KUKOMALIA KATIBA MPYA MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA
    Next Article WAZIRI MKENDA MAONI YA WADAU KUBORESHA ELIMU TUNAFANYIA KAZI AZINDUA MRADI MKUBWA WATRILIONI 1.15

    Related Posts

    SERIKALI YAFUNGIA MGODI WA GEM AND ROCK VENTURE ULIOKO MIRERANI

    March 20, 2023

    TRA CHUNYA KUSAMBAZA ELIMU YA MLIPA KODI KWA WACHIMBAJI WA DHAHABU.

    March 16, 2023

    Wizara ya Madini imefanikiwa kutaifisha madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 4 yenye thamani ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture

    March 16, 2023

    DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

    March 16, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.