Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Break News»Mitambo ya KMTC iko salama na inafanya kazi.

    Mitambo ya KMTC iko salama na inafanya kazi.

    0
    By arushatv on May 30, 2022 Break News

     

    Na Mwandishi wa A24Tv Arusha

    Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amesema mitambo iliyopo katika Kiwanda cha Kilimanjaro Machine tools (KMTC) iko salama na inaendelea kufanya kazi ya uzalishaji wa vipuri na mashine mbalimbali wakati maboresho ya kuendesha mitambo hiyo kielektroniki yanaendelea.

    Waziri Kijaji ameyasema hayo alipofanya ziara katika Kiwanda cha KMTC kichopo Moshi Mkoani Kilimanjaro Mei 29, 2022 kujionea jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi na mikakati iliyopo ya kukifufua ili kifanye kazi kwa ufanisi na kuzalisha bidhaa zinazokidhi mahitaji ya soko kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

    Akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah  pamoja na wajumne wengine aliziagiza Taasisi za TEMDO na CAMARTEC  kufanya kazi kwa kushirikiana na kiwanda hicho ili kiweze kuzalisha bidhaa kwa wingi zilizosanifiwa na Taasisi hizo.

    Aidha, Waziri Kijaji alisema uboreshaji wa Kiwanda hicho ni muhimu kwa kuwa bidhaa za chuma zinahitajika katika matumizi mbalimbali ya kutengenezea mitambo, vipuru na bidhaa  katika miradi ya kimkakati kama  vile Reli ya Kisasa ya SGR  na viwanda vingine vikubwa na vidogo.

    Naye Mkurugenzi  Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) Dkt. Nicolaus Herman Shombe amesema Serikali inaendelea kutekeleza Mkakati wa kufufua kiwanda hicho cha KMTC kinachozalisha bidhaa na vipuri mbalimbali vinavyotumika katika viwanda vingine. Kiwanda hicho kina ukubwa wa eneo la hekari 645 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vingine vitakavyokuwa vinatumia bidhaa za kiwanda hicho.

    Akieleza umuhumu wa kufufua kiwanda hicho  kwa Waziri Kijaji, Meneja Mkuu wa KMTC Bw. Adrian Nyabuki  amesema mipango yote iliyowekwa ya kufufua kiwanda hicho ikitekelezwa itaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa uagizaji wa vipuli na baadhi ya bidhaa za chuma nje ya nchi na kufanya vipuri na bidhaa hizo kupatikana kwa urahisi,  kutoa ajira na kuchangia katika pato la taifa.

    Wakati huo huo, Waziri kijaji akiwa ameambatana na ujumbe wake alitembelea Kiwanda cha kutengeneza magurudumu cha Arusha ( General Tyre ) kujionea mahitaji na mikakati iliyopo ya kufufua kiwanda hicho ili kiweze kuzalisha bidhaa zinazokidhi mahitaji ya soko kwa kutumi

    Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) akitembelea Kiwanda cha Kilimanjaro Machine tools (KMTC)  Mei 29, 2022 kujionea jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi na mikakati iliyopo ya kukifufua ili kifanye kazi kwa ufanisi na kuzalisha bidhaa zinazokidhi mahitaji ya soko kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

    Post Views: 85
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleMAKADA WA CCM ARUSHA WAMVAA MBUNGE GAMBO! MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA24TV
    Next Article Maonyesho ya Kili fair kuanza Rasmi tarehe 3 hadi 5 juni 2022

    Related Posts

    MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AMETOA MILION 33 KUNUNUA UNGA WA LISHE KWA WENYE MAHITAJI MAALUM

    February 9, 2023

    KOREA KUSINI NA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA WALETA PIKI PIKI MPYA ZA KUTUMIIA UMEME

    February 5, 2023

    BREAKING NEWS : MUSA JUMA MWENYEKITI MPYA JOWUTA SERIKALI YAAHIDI USHIRIKIANO

    January 29, 2023

    WAFANYA BIASHARA SAMUNGE JIJINI ARUSHA WAPOKEA MILLIONI 100 KUTOKA KWA NABII MKUU GEORDAVIE WAHIDI MAKUBWA KATIKA KUKUZA MITAJI YAO

    January 27, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.