Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Siasa»HUKUMU YA SABAYA YAGONGA MWAMBA MPAKA JUNI 10 2022

    HUKUMU YA SABAYA YAGONGA MWAMBA MPAKA JUNI 10 2022

    0
    By arushatv on May 31, 2022 Siasa
    Na Mwandisho wa A24Tv
    SBAYA PICAliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya akishuka kwenye gari la Magereza akiingia Mahakamani
    Arusha.
    Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imeahirisha hukumu ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita kutokana na Hakimu kuwa na majukumu mengine.
     Akiahirisha kesi hiyo leo Jumanne Mei 31, 2022, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Fadhil Mbelwa amesema shauri lilipangwa kwa ajili ya hukumu ila hakimu aliyekuwa akiisikiliza amepangiwa majukumu mengine ya kikazi nje ya ofisi.

    “Shauri linakuja kwa ajili ya hukumu na liko kwa Hakimu Mkazi Mwandamizi, Patricia Kisinda lakini siku ya leo amepangiwa majukumu mengine ya kikazi nje ya ofisi hataweza kutoa hukumu leo hadi Juni 10, 2022,” amesema Hakimu huyo

    Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 27/2021, mbali na Sabaya watuhumiwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

    Leo Jamhuri iliwakilishwa na Mawakili wa Serikali waandamizi Janeth Sekule, Felix Kwetukia, Wakili wa Serikali Neema Mbwana na Mwendesha Mashitaka wa Takukuru, Jacopiyo Richard.

    Utetezi uliwakilishwa na Mawakili Mosses Mahuna, Fridolin Bwemelo, Edmund Ngemela na Sylvester Kahunduka ambao wanawatetea washitakiwa sita isipokuwa Mwahomange ambaye anajitetea mwenyewe mahakamani hapo

    Post Views: 106
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleSABAYA KUSUKA AU KUNYOA LEO KESI YA UHUJUMU UCHUMI MAGAZETI YA LEO ARUSHA 24TV
    Next Article BEI MPYA YA MAFUTA YALETA MATUMAINI MAGAZETI YA LEO NA ARUSHA 24TV

    Related Posts

    MRITHI WA MREMA WA TLP KUPATIKANA KESHO UCHAGUZI WAPAMBA MOTO

    March 5, 2023

    CCM NA SERIKALI SAMBAMBA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI IKUNGI

    January 17, 2023

    JUMUIYA YA WAZAZI TAIFA YAMPONGEZA RAIS SAMIA TAMKO LA MIKUTANO YA HADHARA

    January 4, 2023

    MIKUTANO YA HADHARA RUKSA IGP WAPE VIBALI MUDA WOWOTE

    January 3, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.