Facebook Twitter Instagram
    Facebook Twitter Instagram
    A24TV News
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    A24TV News
    Home»Habari»ASKOFU MPYA ASIMIKWA NA MSAIDIZI WAKE KANISA LA KKAM

    ASKOFU MPYA ASIMIKWA NA MSAIDIZI WAKE KANISA LA KKAM

    0
    By arushatv on May 29, 2022 Habari

     

    Askofu Philemon Mollel akisimikwa kua Askofu

    Na Geofrey Stephen Arusha

    Kanisa la kilutheri Afrika Mashariki(KKAM) limewasimika na kuwaingiza kazini watumishi wawili amabo ni mchungaji Dr Philemon Langas Molel kuwa Askofu wa Jimbo la Arusha Mashariki pamoja na mch Dr Philemon Olaisi Molel (MONABAN) kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo Hilo .

    Askofu mkuu wa kanisa Hilo Askofu Osca John Olotu akizungumza katika ibada ya kuwasimika watumishi hao ;iliyofanyika maeneo ya Ngulelo ,amesema kuwa wametimiza agizo la Mungu aliloagiza la enendeni ulimwenguni mkahubiri Injili.

    Amesema kuwa ili kusudi Hilo litimie lazima wahubiri Injili kupitia utumishi waliopewa hivyo kupitia watumishi hao wanatarajia waumini kuongezeka na wanatarajia kufikia vijiji vyote ili kupeleka Injili.

    Ameongeza kuwa wao hawatafanya mashindano ya aina yeyote badala yake watasimamia kusudi moja la kuhubiri Injili ya Yesu Kristo.

    Akizungumza Mara baada ya kuingizwa rasmi kazini Askofu Dr Philemon Langas Molel amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa daraja jipya alilolipokea na wajibu walio nao ni kuhakikisha wanaotesha makanisa sehemu mbali mbali.

    Ameongeza kuwa kanisa Hilo na mengine hayana tofauti kwani yote yanalenga kumhubiri Yesu Kristo lakini tofauti ndogo ikiwa ni kutowabariki wanawake kuwa wachungaji.

    Kwa upande wake msaidizi wa Askofu mchungaji Dr Philemon Olaisi Molel (MONABAN)akiongea Mara baada ya kubarikiwa na kuingizwa kazini amesema kuwa amesikia furaha Sana kwani kanisa Hilo linahubiri Amani na ushirikiano

    ‘Kanisa letu tutakuwa tunahubiri upendo Amani, ushirikiano na umoja katika maeneo yote nchini na hata kwenye nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki.”ameisisitizia Monaban

    Monaban Amedai kuwa kwa kuwa Mungu amempa vipawa viwili ikiwemo Cha Siasa pamoja na utumishi wa madhabauni atavitumia vyote kwa pamoja kwa kuwa atawahidumia watu wake kiroho na kimwili na atahakikisha anavitumia vizuri Kama Mungu alivyokusudia.

    Katibu wa kanisa Hilo Afrika Mashariki Heroki Mkwizu amesema kuwa parokia nyingi kwa Sasa zitafunguliwa Arusha pamoja na maeneo mengine Mara baada ya kuongezeka kwa watumishi hao

    Mwisho

    Post Views: 549
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr WhatsApp Email
    Previous ArticleMAGAZETI YA LEO NA ARUSHA24TV CAG SIOGOPI CHOCHOTE
    Next Article Kada wa Ccm na Mfanya Biashara Maarufu Ashinda uchaguzi wa Tawi kwa Kishindo

    Related Posts

    Tanzania na India kuendeleza Uhusiano wa Kibiashara na Uwekezaji

    March 27, 2023

    TANZANIA YAKABILIWA NA UHABA WA MABAHARIA VIJANA.

    March 27, 2023

    Marcas Ajitosa kuwania U NEC Arusha

    March 25, 2023

    VIKUNDI 47 KUPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI MOITA MONDULI

    March 24, 2023

    Leave A Reply Cancel Reply

    Facebook Twitter Instagram Pinterest
    • Home
    • Habari
    • Magazeti
    • Break News
    • Siasa
    • Burudani
    • Makala
    • Michezo
    © 2023 a24tv. Designed by Ishimax Ltd.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.