Author: John Walter

Na John Walter -Kiteto Mahakama ya Wilaya Kiteto mkoani Manyara, imemhukumu MAMBE MOHAMED MAMBE,  Mwenyekiti wa Kijiji cha Nasetan, Kata ya Engusero. Mshtakiwa ametiwa hatiani na kuamriwa kwenda Jela miaka minne au kulipa faini ya shilingi 1,000,000/= kwa makosa ya kuomba na kupokea hongo kiasi cha shilingi  60,000/= kinyume na k/f 15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 kama ilivyofanyiwa marejeo Mwaka 2022. Hukumu hiyo dhidi ya MAMBE MOHAMED MAMBE  katika kesi ya jinai Na.20/2023, imetolewa na Mhe. Boniface Lihamwike, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kiteto, Machi 27, 2024. Mshtakiwa aliomba hongo ya…

Read More

Na John Walter-Babati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imemaliza ziara yake ya siku tatu  katika mkoa wa Manyara kwa kutembelea jengo la utawala la halmashauri ya wilaya ya Babati na nyumba ya mkurugenzi ambayo ipo katika hatua ya ujenzi. Baada ya kukagua majengo hayo LAAC imetoa mapendekezo yafuatayo. Mkurugenzi ahakikishe fedha zilizobaki kiasi cha  shilingi Milioni 103 zinatumika kukamilisha mradi kufikia tarehe 10 mei,2024 kama ilivyoanishwa katika mkataba na sio kuomba fedha za nyongeza ofizi ya Rais TAMISEMI. Aidha ofisi ya Katibu tawala (RAS) mkoa wa Manyara  ifanye tathmini ya kina juu ya…

Read More

Na John Walter-Babati Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na utoaji elimu ya utunzaji wa Mazingira na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia wilaya ya Babati (BAMBAGO FOUNDATION) wamesherehekea siku ya wanawake duniani kwa kutoa elimu katika maadhimisho yaliyofanyika tarafa ya Bashnet kata ya Madunga Halmashauri ya wilaya ya Babati. Akizungumza na wananchi hao mratibu wa BAMBAGO FOUNDATION Lucy Sylvester, aliwasihi wananchi kuripoti vitendo vya Ukatili  vinapotokea katika maeneo yao na kuwa Karibu na watoto wao. Mratibu aliambatana na katibu wa Shirika hilo wilaya ya Babati Deogratius Gwasma ambaye alifafanua kuwa suala la Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia vimekuwa tishio kubwa…

Read More

Na John Walter-Babati Akina Mama wa Kata ya Riroda wilayani Babati mkoani Manyara, wamesema wamechoshwa na vitendo vya kubakwa na kuporwa mali zao na watu ambao bado hawajafahamika hali inayowapa hofu ya kwenda maeneo ya mlimani kutafuta kuni. Wakizungumza katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na mkuu wa wilaya Lazaro Twange kwa lengo la kusikiliza kero na kuzitafutia majibu akiwa na idara mbalimbali, wamesema watoto wa shule pia wanakumbana na vitendo hivyo vya ukatili kwani wapo baadhi wamekatisha masomo yao kwa kupewa ujauzito na watuhumiwa hawajakamatwa mpaka sasa. “Tukiamka salama tunashukuru Mungu, watoto wetu wa kike wakienda shule tunafofu, sisi twende…

Read More

NJOO UNUNUE SETI MPYAA YA KUFUA UMEME KATIKA MGODI WAKO… HII SET NDIO SURUHISHO LA UMEME KATIKA MGODI WAKO: Piga 0692711353 BEI YA SETI HII: TSH 4,000,000/= Wale ambao wanatafuta namna ya kuleta umeme wa 3-PHASE (UMEME MKUBWA WA VIWQNDANI) katika mgodi yao basi seti hii hapa ndio SURUHU YENU kwani kwa seti hii unayoiona hapa inatosha kabisa kuzalisha umeme wa 20KW ambao utatosha kuendeshea pump katika mgodi wako, kuendeshe na mashine zingine zinazotumia umeme…. UKINUNUA HII SETI NI SAWA UMENUNUA MGODINI KWAKO GENERETA KUBWA KABISA LA UMEME MGODINI KWAKO AU NI SAWA NA KUVUTA UMEME WA TANESCO MGODINI KWAKO……

Read More

Na John Walter-Manyara Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange amewapongeza viongozi wa Dini nchini kwa juhudi zao za kuendelea kupambana na vitendo vya ukatili na kuahidi kuwa,Serikali itaendelea kushirikiana nao vyema katika kuhakikisha vinatokomezwa katika maeneo yote nchini. Twange ameyaeleza hayo leo machi 2,2024 mjini Babati alipomwakilisha mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa Bazara la Waislamu Tanzania (BAKWATA ) mkoa wa Manyara uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa Manyara. Amesema viongozi wa dini wanayo nafasi kubwa ya kuelimisha wananchi kuwa na hofu ya Mungu na hivyo kuepuka…

Read More