Site icon A24TV News

Wakulima washauriwa kuwekeza viwandani

Njombe
Na Emmanuel octavian

Wakulima mkoani Njombe wameshauri wawekezaji waachane na biashara ya kuwekeza mashambani na badala yake wawekeze kwenye viwanda vitakavyowasaidia wao kupeleka mazao yao.

Katika mkutano mkuu wa mtandao wa vikundi vya wakulima MVIWATA Tanzania katika mikoa ya Njombe na Iringa baadhi ya wanachama hao ambao ni wakulima wanasema kitendo cha wawekezaji kwenda kuwekeza mashambani kinawanyima fursa wakulima ambao ndio wahusika wakuu katika sekta ya kilimo.

Hosea Mangula,Sikujua Mbata,John Kiswaga na Sarah kaduma ni baadhi ya wakulima wanaosema wawekezaji wanaoingia mashambani kuwekeza pia wanasababisha kuibuka kwa migogoro ya ardhi inayochochea chuki baina ya wakulima, Wawekezaji na serikali inayowaruhusu wawekezaji hao kuingia kwenye sekta ya Kilimo.