Site icon A24TV News

WAKALA WA MISITU WAPANGA KUKUSANYA BILION 3.7

Na Geofrey Stephen Lushoto .

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), kupitia shamba la Miti la  Shume,lililopo Wilayani Lushoto, Mkoa wa Tanga katika mwaka wa fedha 2022/23 imepanga kukusanya mapato ya serikali ya shilingi Bilioni 3.7.

Makusanyo hayo yanatokana na mauzo ya mazao ya miti na zao la nyuki  .
Akiongea na waandishi wa habari waliotembelea shamba hilo katika ziara ya Mkuu wa wilaya ya Lushoto,Kalisti Lazaro,Mhifadhi Mwandamizi wa Shamba hilo,Ernest Madata alisema mwaka wa fedha 2020/21 walishindwa kufikia malengo ya kukusanya sh,bilioni 3.8 waliojiwekea na kukusanya sh,bilioni 2.2 sawa na asilimia 59.4.
Alisema kutofika kwa malengo hayo  kulichangiwa na changamoto  mbalimbali ikiwemo kushuka kwa zao la mbao na Nyuki kulikochangiwa na janga la UVIKO-19.
Mhifadhi huyo alisema kuwa changamoto hiyo ilipelekea kushuka pia kwa  malengo ya makusanyo ya halimashauri ya sh,miliojin108 na kufanikiwa  kukusanya sh,milioni 74.5 tu sawa na asilimia 68.49.
Alisema mwaka huu wa fedha 2022/23 wamepanga kuvuka lengo la makusanyo kwani hadi hivi sasa wameshafikia asilimia 16 ya makusanyo jambo ambalo alidai watavuka malengo waliojiwekea.
Madata alisema Shamba la Shume ni moja kati ya mashamba makubwa ya miti yanayomilikiwa na TFS lenye ukubwa wa ekari 4863 ambalo lilianzishwa mwaka 1926 kwa lengo la kuendeleza shughuli za upandaji miti kwa ajili ya utunzaji wa mazingira na ukusanyaji wa maduhuli ya serikali.
Pia alisema faida ya shamba hilo ni pamoja na kutoa kwa ajira kwa wananchi wilayani humo ambapo kwa mwaka  wananchi wapatao 200,000 wananufaika na ajira na hivyo kujiongezea kipato.
‘Uwepo wa shamba la miti wilayani Lushoto katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita 2020/2021 wamechangia sh,milioni 260 kuboresha miundombinu ya barabara yenye urefu wa kilometa 14.4 iliyopo katika jamii inayowazunguka “
Awali mkuu wa wilaya Lushoto, Kalisti Lazaro aliipongeza TFS kwa kuchangia maendeleo wilayani huo na kuitaka kuongeza jitihada zaidi ili kufikia malengo waliyojiwekea .
Lazaro alisema kuwa TFS kupitia shamba hilo imechangia kupunguza suala la ajira wilayani humo hususani vijiji vinavyozunguka shamba hilo na kuwataka wananchi kulitumia shamba hilo kuongeza vipato vyao na kukuza uchumi wa taifa.
Ends…