Site icon A24TV News

Vijana 20 wakopeshwa pikipiki bila riba na Halmashauri ya Wilaya Makete

Halmashauri ya Wilaya ya Makete kupitia 10% ya mapato yaa ndani imewakopesha vijana pikipiki (bodaboda) 20 kutoka Kata ya Kitulo na Iwawa.

Kati ya vijana hao 20, vijana 10 ni kutoka Kata ya Iwawa na Vijana 10 ni kutoka kata ya Kitulo…Mkopo huo ni kiasi cha shilingi Milioni 51 na zitarejeshwa kwa kipindi cha mwaka mmoja bila riba.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika Viwanja vya ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Makete mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda, Makamu wa Halmashauri Mhe. Hawa Kader, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya William Makufwe, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ndg. Clement Ngajilo, waheshimiwa Madiwani, wakuu wa Idara na vijana wa Kitulo na Iwawa