Site icon A24TV News

NABII MKUU GEORDAVIE AGAWA MISAADA NCHINI BURUNDI APEWA TUZO YA HESHMA

Na Geofrey Stephen A24Tv

Nabii Mkuu Mh GeorDavie  Amekabidhiwa Tuzo ya Heshima Nchini Burundi itwayo Mandela Peace Center   kwa kutambua mchango wake katika kusaidia jamii yenye uwitaji .

Akiwa nchini Burundi Mh Nabii Geordavie Amekabidhiwa Tuzo iyo kama Baba wa Amani Duniani kwa kutambua Mchango wake wa kusaidia jamii katika mambo mubimu ikiwemo  watu wenye matatizo mbali mbali na wenye uwitaji .

Pamoja na tuzo hiyo Nabii Mkuu Mh Geordavie alipata Fursa ya kukutana na viongozi mbali mbali nchini humo kwa mazungo ambapo alielezea ziara yake ilivyo lenga kuwagusa wenye maitaji.

Amesema yeye kupewa tuzo iyo imemuongezea kufanya kazi zaidi katika kuwanyanyua watu wenye uwitaji kwani pamoja na kuhubiri injili lakini pia ameguswa kusaidia watu wenye uwitaji hasa katika kupata mitaji ya kuendesha maisha yao 

Nabii Mkuu amesema ataendelea kusaidia wasio jiweza kwani katika uduma yake ameanza kuwaudumia watu amekutana na wenye changamoto kubwa hivyo akaona ni vyema kuwashika mikono katika maisha yao .

Nabii Mkuu GeorDavie ameendelea kugusa Maisha ya Mamia kwa Maelfu ambapo sio kwa Tanzania tu ambapo uduma yake inapo patikana na sasa amevuka mipaka na kwenda nje ya nchi kusaidia na kuwagusa jamii yenye uhitaji .

Mbali na ziara iyo Nabii Mkuu amewafungua na kuwatamkia baraka wananchi wa nchini Burundi kila jambo ambalo watakalo gusa na kufanya jambo la maendeleo wabarikiwe na wasirudi nyuma bali wafanikiwe kusonga mbele zaidi .

Mwisho .