Site icon A24TV News

MWINJILISTI WA KANISA LA MATAIFA YOTE APATA MAONO LENGAI OLE SABAYA KUACHIWA HURU ATAKUA KIONGOZI TENA

Mwinjilist Eva Kaaya wa kanisa la Mataifa yote amepata
Maono kutoka kwa Mwenyezi Mungu aliyempa juu ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai  Mkoani kilimanjaro Lengai Ole  sabaya .

Akizungumza na A24tv Mwinjilisti Eva Amesema kwamba wakati akiendelea na Maombi Mungu akamuonyesha  amemridhia na anaenda kumtoa kwenye vifungo na mashtaka yote ndani ya wiki moja kuanzia tarehe. 15 November 2022.

Mwinjilisti wa kanisa la Mataifa yote Eva kaaya  amefafanua kwamba maono hayo ambayo Mungu amemuoyesha ni kwamba Damu ya Yesu imemsafisha na atakua safi kwa  hivyo atatoka katika vifungu na kua huru .

Amesema kwamba kwa Sabaya Atarudi tena madarakani baada ya muda akiwa kiongozi mpya katika Kristo.
Haya ndiyo maono aliyonionyesha Yesu Kristo alfajiri ya tareha 15 November 2022.

Hivi karibu kumekuwepo na mamneno kwamba Legai Ole Sabaya wenda akaachiwa kua huru mara baada ya kukubaliana na masharti ya kukiri makosa yanayo mkabili mara baada ya ya wafuasi wake kumtangulia kukiri na kupigwa faini na kuachiwa wacha tuone maono ya Mwinjilisti Eva wa makani yote ya kimafaifa

Mwisho