Site icon A24TV News

MKUU WA WILAYA MAKTABA SASA ZIWE KATIKA MFUMO WA KIMTANDAO KWENDANA NA KASI YA TEKNOLOJIA

Na Geofrey Stephen  Arusha

MKUU wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango amewataka watunzi wa vitabu  vya elimu hapa nchini ,kuanza mabadiliko ya kuingiza machapisho ya vitabu  kwenye  mfumo wa maktaba mtandao ili kuwafikia wasomaji  waliowengi kupata taarifa kwa gharama  nafuu
Mkuu huyo wa wilaya ameyasema hayo jijini Arusha wakati akizindua mfumo  wa usomaji wa vitabu mtandaoni katika chuo cha uhasibu Arusha (IAA)  unaoratibiwa na shirikisho la Maktaba za vyuo vikuu na taasisi zilizofanya utafiti COTUL.
“Tunataka vitabu vyote vinavyotungwa na watunzi wetu hapa nchini wakiwemo maprofesa vionekane kwenye Mtandao ili elimu yetu hapa nchini iweze kusomeka kwenye mfumo wa kidunia”
Naye kaimu mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha,dkt Cairo Mwaitete alisema kuwa mfumo wa kuingiza machapisho kwenye mtandao kutapunguza gharama za kupata taarifa hususani kwa wanafunzi waliopo nje ya nchi

Alisema mabadiliko hayo yatakwenda kupanua wigo kwa wasomaji kupata taarifa za ndani wakiwa nje ya nchi na kuongeza ushindani wa elimu duniani. 

“Kupitia Cotul kutasaidia watanzania wote kuwa  na uwezo wa kupata taarifa kwa gharama nafuu,tunaomba wizara ya elimu iwezeshe miundo mbinu  ili gharama za uchapishaji ziwe nafuu”
Kwa upande wake Mkurugenzi  mkuu wa bodi ya huduma za maktaba, dkt. Mboni Amiri alisema kwa sasa bodi ya huduma za maktaba ipo katika hatua ya kuhama kutoka maktaba za kawaida na kuingia kwenye mfumo wa kielekitroniki. 

“Kwa sasa tupo mbioni kutengeneza sera ya kitaifa ya huduma za maktaba nchini ambayo haikuwepo ili kusimamia haki za machapisho ya watunzi”

Naye mwenyekiti wa Cotul,Sydney Msonde alisema kuzinduliwa kwa mfumo huo ni kutokana na mabadiliko  ya kidunia kutoka analogi na kwenda kidigtal.

 

Alisema matarajio ni kuona machapisho ya kisayansi ya watafiti yanaweza kufundishwa kwa mfumo wa kielekitroniki na kuwafikia wasomi wengi zaidi duniani.

 

Awali profesa Alfred  Sife, makamu mkuu wa chuo cha ushirika Moshi alizitaka maktaba zote hapa nchini kuboresha huduma zake  ili ziendane na mabadiliko ya sayansi na teknolojia na hivyo kupanua wigo wa kutoa huduma duniani .

Wageni waliofika katika uzinduzi huo wakifatilia mjadala kwa umakini .