Site icon A24TV News

MAKAA YA MAWE YATAJWA KUPANDA BEI MARA DUFU KUTOKANA NA VITA VYA UKRAINE NA URUSI

Na Mwandishi wa A24Tv .

Dkt Fredrick Gilenga afisa madini mkoa wa Njombe amesema Kutokea kwa vita vya Ukraine na Urusi kumepelekea uhitaji mkubwa wa madini ya makaa ya mawe na kupelekea bei yake kupaaa zaidi.

Dkt.Gilenga ametoa kauli hiyo katika kikao Cha ushauri mkoa wa Njombe RCC ambapo amesema uwepo wa makaa ya mawe mkoani Njombe Ni fursa kubwa inayoweza kuuingizia mkoa fedha nyingi za kigeni.

Makaa ya mawe kwa mkoa wa Njombe yanapatikana Wilaya ya Ludewa ambayo yanaweza kuchimbwa kwa miaka 100 huku wawekezaji wakitaja changamoto kubwa ya miundombinu ya barabara kuwa ni kikwazo.