Site icon A24TV News

LATRA ARUSHA SASA NI LESENI ZA MAGARI MAKUBWA YA ABIRIA WAMILIKI WAJIPANGE

Na Geofrey Stephen Arusha 
MAMLAKA ya Udhibiti ,Usafiri Ardhini (LATRA)mkoa wa Arusha imetangaza kusitisha kutoa leseni kwa magari madogo ya abiria aina ya Haice na Noar katika jiji la Arusha na kuwataka wamiliki wa magari hayo ya biashara kujipanga kwa kununua magari makubwa.
Aidha amewataka wasafirishaji kuzingatia mwongozo wa serikali kwa kutoa tiketi mtandao kwa mfumo wa kielekitroniki na wale wanaoendelea kukaidi wajiandae kisaikolojia kuoigwa adhabu kali.
Akiongea katika ziara ya naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi, Atupele Mwakibete ambaye alitembelea  ofisi za mamlaka hiyo jijini hao,meneja wa Latra Mkoa wa Arusha,Amani Mwakalebela alisema kuwa mamlaka hiyo imesitisha kutoa leseni kwa magari madogo ya abiria kutokana  na magari hayo  kutokuwa rafiki na hadhi ya jiji.
Alisema kuwa Latra imeweka mpango mzuri wa usafiri na usafirishaji kwa kuyaondoa taratibu magari madogo aina ya haice ili kuruhusu usajiri wa magari makubwa yatajayoendana na hadhi ya jiji kwa kuwa mji umekuwa.
“Tumesitisha kutoa leseni kwa magari aina ya Haice kutoa huduma katikati ya jiji kwa kuzingatia mahitaji ya jiji “
Aliwataka wafanyabiashara wa magari ya abiria kununua magari makubwa yenye uwezo wa kupakia abiria wengi na yatapewa leseni ya kusafirisha abiria umbali wowote.
Akizungumzia magari aina ya Noar yanayosafirisha abiria kwenda wilaya ya Karatu na Namanga alisema kuwa Latra imesitisha kutoa leseni ya magari hayo ila iliruhusu baadhi ya magari aina ya Noar ambayo tayari yalikuwa yameshafika nanyakitoa huduma ya usafirishaji kabla ya kusitisha zoezi la utoaji wa leseni .
Akizungumza katika ziara hiyo naibu waziri Mwakibete aliipongea Latra kwa utendaji kazi na kuwataka kuhakikisha wanasimamia sheria ikiwemo kusomiliza changamoto za wasafiri na wasafirishanj.
Aidha alitoa rai kwa Latra mkoani hapa kuhakikisha inatoa elimu zaidi katika sekta ya usafirishaji jambo litakalosaidia kuondoa malalamiko yasiyo na tija