Site icon A24TV News

WANANCHI WAFUKUZA DAKTARI KISA ULEVI NA MAJIBU MABOVU

Njombe

Wananchi wa kijiji cha Igombola kata ya Lupembe wilayani Njombe wameomba serikali kupitia Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa kuondoka na mganga wa zahanati ya kijiji hicho wakimtuhumu kukosa nidhamu,ulevi pamoja na kushindwa kutibu wagonjwa mpaka watoe fedha za matibabu wakiwemo wazee.

Katika mkutano wa hadhara wa Mkuu wa wilaya hiyo wakati akisikiliza kero pamoja na kukagua miradi ya maendeleo,wananchi wamedai kuwa daktari Samweli Tupa amekuwa na changamoto zinazopelekea vifo kwa wagonjwa hali inayowafanya kuwa na wasi wasi mkubwa wa maisha yao ndio maana wamefikia hatua ya kuomba aondolewe

Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa mara baada ya kusikiliza changamoto hiyo ametoa maelekezo kwa mganga mkuu wa halmashauri hiyo Dkt,Suke Magembe kumuondoa daktari huyo mara moja huku mganga Mkuu wa halmashauri akikili kuwa tayari wamekwishachukua hatua za kumuondoa mtumishi huyo na kumrudisha makao makuu.

“Maelekezo yangu,kama mtumishi huyu ana barua leo uondoke naye ili isiendelee kuwa kero,lakini mtu kama huyu ambaye ana tabia mbovu na kukiuka maadili ya kazi kumuamisha sio adhabu sasa ili tusimuonee mtu afunguliwe mashtaka kwa mujibu wa sheria za utumishi ili kama habadiriki atupishe aachie wengine wanyenyekevu kwasababu tutampeleka tena sehemu nyingine wananchi tena wanamkataa”amesema Kissa Kasongwa