Site icon A24TV News

DC LUSHOTO KALIST, AMVAA VIKALI MKANDARASI! ALIYEKWAMISHA MRADI WA MAJI WA BILIONI 1.8

Na Geofrey Stephen ,Lushoto
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga,Kalist Lazaro amewataka Wakurugenzi wa Kampuni ya M/S PNR SERVICES ya Jijini Dar es Salaam waliopewa zabuni ya shilingi Bilioni 1.8 ya kuvuta maji km 14 kutoka
Hifadhi ya Msitu wa Magamba hadi katika Mji wa Lushoto kujisamilisha wenyewe ofisini kwake kwa nini hadi Sasa wameifanya kazi hiyo kwa asilimia 20 tu.

wakati mradi huo wanapaswa kuukabidhi kwa Mamlaka ya maji Lushoto(RUWASA) januari 30 mwaka kesho.

Lazaro alisema hayo katika chanzo Cha maji Cha Msitu huo alipotembelea Mradi huo na kusikitishwa kuona Mkandarasi amelipwa zaidi ya shilingi milioni 200 kwa ajili ya kazi hiyo lakini amekuta wafanyakazi saba tu

katika ujenzi wa chanzo Cha maji Hali iliyomsikitisha na kupata taarifa kuwa Wakurugenzi wa Kampuni hawajawahi fika Lushoto pamoja na kutakiwa na uongozi wa RUWASA zaidi ya Mara tatu.
Mradi wa ujenzi wa maji ukionekana katika ujenzi kwa asilimia% 20 
Alisema na kumwagiza msimamizi wa mradi wa Kampuni hiyo, Singo Omari aliyemkuta eneo la Mradi kuwataarifa Wakurugenzi wake kuwa anawahitaji
haraka ofisni kwake Alhamis  octoba 27 mwaka huu saa 1.30 asubuhi kufika bila kukosa  kujieleza Ni kwa Nini wasichukuliwe hatua kwa kupuuza wito wa Meneja

wa RUWASA Wilaya ya Lushoto na kwa nini kazi haifanyiki wakati wameshachukua mamilioni ya pesa za Serikali kwa ajili ya Mradi huo.

Mkuu wa Wilaya alisema tanki ya maji lenye uwezo wa kubeba Lita 600,000 bado halijajengwa,usambazaji wa bomba za maji za umbali wa km 14 kutoka Msitu wa Magamba hadi Mjini Lushoto bado mtaro haujachimbwa Wala mabomba hayajafika eneo la Mradi na alisema dharau za Wakurugenzi wa Kampuni ya M/S PNR SERVICES waliifanya haitavumiliwa kamwe lazima
waeleze ni kwa nini muda wote hawajafanya kazi na pesa ya Serikali wameshapewa.

” Waambie Wakurugenzi wako nawahitaji ofisini kwangu Alhamis asubuhi
saa 1.30 hii haikubaliki na sitakubali Wilaya niliyokabidhiwa na Rais
Mkandarasi afanye anavyotaka katika Miradi ya Maendeleo  hii
haikubaliki hatua lazima zichukuliwe ” alisema Lazaro

Naye Meneja wa RUWASA katika Wilaya ya Lushoto, Erwin Sizinga alisema kuwa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo hawana ushirikiano na ofisni yake kwani wamekuwa wakifanya kazi wanavyotaka na kutoa sababu nyingi zisizokuwa na Msingi toka walipopewa kazi hiyo March Mwaka huu pamoja
na kupewa kiasi Cha zaidi ya shilingi milioni 200 walizoomba katika malipo ya awali.

Meneja wa Ruwasa akizungumza na waandishi wa habari ya juu ya mradi huo kusua sua 

Sizinga alisema mahitaji ya maji katika wilaya ya Lushoto ni lita milioni 12.3 kwa siku na kwa sasa lita milioni 8.3 kwa siku maji yanatoka na kuna upungufu wa maji lita milioni 3.9 kwa siku na iwapo miradi yote itakamilika kuna uwezekano mkubwa wa kupatikana kwa maji kwa wingi katika wilaya hiyo.

Alisema Mji wa Lushoto una hitaji Sana maji kutoka chanzo Cha Msitu wa Asili wa Magamba na Mradi huo ukikamilika una uwezo wa kutoa Lita 150,000 hadi 160,000 kwa saa kutoka katika chanzo hicho na Mradi huo ukikamilika huenda shida ya maji katika Mji wa Lushoto na wenye kata 51 na vijiji 208 ukaisha.

Alisema Changamoto ya maji katika wilaya ya Lushoto kwa Sasa ni asilimia 68 na iwapo Miradi yote ya maji ikikamilika Changamoto hizo zitakwisha na maji yatakuwa mengi katika Wilaya hiyo yenye biashara
kubwa ya matunda na mboga mboga.

Naye Meneja wa Kampuni ya M/S  PNR SERVICES ,Omari Singo alikiri kutokamilkika ndani ya muda kwa mradi huo na kumwomba Mkuu wa Wilaya kumpa muda zaidi ili aweze kuzungumza na Wakurugenzi wa Kmapuni hiyo ili waweze kumpa ,ajibu sahihi juu ya mradi ili unaweza kukamilika.

Mwisho