Site icon A24TV News

MARUFUKU KUWALISHA MAKANDE WATOTO KILA SIKU

 

Na Emmanuel octavia

Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amewataka wananchi  kuachana na mtindo wa kula chakula Cha aina moja hususani Kan
de wakati wote kwani kunachangia kwa kiasi kikubwa kushamiri kwa udumavu.

MARUFUKU KUWALISHA MAKANDE WATOTO KILA SIKU

Kasongwa ametoa kauli hiyo akiwa katika vijiji vya Itunduma na Sovi kata ya mtwango katika ziara yake ya kijiji kwa kijiji katika halmashauri ya wilaya ya Njombe ambapo amesema kitendo cha watoto kushindia kande wakati wote kinasababisha utapimlo kwao jambo ambalo halifai katika ustawi wa watoto.

Aidha mkuu huyo wa walaya amekiri kuwa wananchi wa wilaya ya Njombe wamekuwa wachapakazi kwelikweli lakini isiwe sababu ya kuwaacha watoto wawe wanakula Cha aina moja ilihali kuna kila aina ya vyakula na matunda ambayo wengi hawayatumii kwa chakula zaidi ya biashara.

Amesema kuna haja ya kuweka msako wa ambao hawali matunda kwani mlo kamili unahusisha matunda kwa asilimia kubwa